Vituko

Vituko

klorokwini

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
8,647
Reaction score
5,145
aahhh vituko hivi vituko, visikieni jamani
jimama kakosa mwiko ,atumia wa jirani
keshazua sokomoko,na gumzo mtaani
hakukitaka kijiko ,alichonacho nyumbani.

mwengine katuchekesha,vioja katuletea
usiku kucha kakesha ,jasho limemuenea
eti mawe achemsha,supu yake aisubiria
hakika alituchosha ,tukaamua kuishia.

na hiki kitendawili ,aah jei efu tegueni
wengi wenye akili,kimewashinda yakini
kapigwa risasi mbili,bado yupo duniani
hazimtoshi; halali ,ya tatu aitamani .

ajabu hii ajabu, kwakweli inashangaza
haking'ari si dhahabu,kimejaa miujiza
wengi wanapata tabu,tena kinawaumiza
wala hakina aibu ,ni wengi kimewakwaza.

na mwisho hii ajali,hakika yasikitisha
nahodha leo kafeli,jahazi kalizamisha
abiria hawakujali ,kuyapoteza maisha
kisha watoa kauli,nahodha kawaridhisha.


hehehehe ni mimi malenga wenu klorokwini a.k.a 2pac wa kigamboni.
 
hii thread toka june 2010replies-0views-793
 
heheh ukiona hivyo ujue hawakuelewa!halaf ilikuwaje kuwaje ukaichimbua? khaaaa! nimeshangaa halaf nikasapraizi
kashairi katamu hako ngoja nikaprinti?hv ukitaka huchukua kitu hadi invisible authorize?
 
kashairi katamu hako ngoja nikaprinti?hv ukitaka huchukua kitu hadi invisible authorize?
Smile bana! haka kashairi mie mwenyewe nilokaandika sikaelewi halaf wewe unataka kukaprint? khaaa!
Halaf hapo red huyo jamaa ana authorize ban tu
 
Back
Top Bottom