vitunguu ni mkombozi

vitunguu ni mkombozi

YUDITHA

Senior Member
Joined
May 5, 2013
Posts
154
Reaction score
28
naomba ushauri wenu jinsi ya kukabiliana na wezi ktk masoko ya dar pale unapoleta vitunguu sokoni bei wanapanga wao
 
naomba ushauri wenu jinsi ya kukabiliana na wezi ktk masoko ya dar pale unapoleta vitunguu sokoni bei wanapanga wao
shkamoo, ninge kushauri utafute wateja kwanza. hangaikia kujua ni nani anahitaji vitunguu na mawasiliano yake harafu mnaelewana bei. zungumza na wateja kadhaa ndio ulete mzigo. wanatabia ya kujipangia bei kwakuwa wanajua hauto weza kurudi na mzigo. pia unapo panga bei lenga kupata faida sio faida ilyo kufuru, usiache kuchukua mawasiliano ya wateja wako. kuwa mcheshi na mkarimu itawajengea kuji heshimu. harafu unaweza kutupatia taarifa za kilimo chako kama kinafanyika wapi, ukubwa gani, kiasi cha mazao, Yako na bei. nashukuru
 
Nashukuru Sana Ndugu. Nimekuwa Nikiangaika Kutafuta Wateja Bado Sijafanikisha Sana Hadi Sasa Nimempata Mmoja. Je Kama Unaweza Kuniunganisha Na Wateja Ikiwa Unawafahamu Nitafurahi Zaidi.
 
Umeulizwa vitunguu vya wapi, aina, kiasi gani? Unajua kuwa muwazi inamvutia mteja hata hapa. Tunaweza hangaika kukutafutia soko kumbe una gunia chache au nyingi sana. Nakutakia heri
 
Asante Mkuu Kwa Ukarimu Wako. Aina Za Vitunguu Red Creoles Ambovyo ni Vikubwa2 Na Size Ya Kati. Ninagunia 90 Kutoka Ruaha Mbuyuni. Mimi Silimi Bali Naingia Kwenye Business Hii Kwa Mara Ya Kwanza Kwa Kukusanya Kutoka Kwa Wakulima Na Kwenda Kuuza Kwa Bei Ya Jumla Dar. Nimeanza Ruaha Mbuyuni, Nitaenda Singida Na Hata Ilula Iringa Na Sehemu Zinginezo. Nimejipanga Kwa Atleast Kila Wiki Niingize Mzigo Dar Kama Nitapata Network Nzuri.
 
Asante Mkuu Kwa Ukarimu Wako. Aina Za Vitunguu Red Creoles Ambovyo ni Vikubwa2 Na Size Ya Kati. Ninagunia 90 Kutoka Ruaha Mbuyuni. Mimi Silimi Bali Naingia Kwenye Business Hii Kwa Mara Ya Kwanza Kwa Kukusanya Kutoka Kwa Wakulima Na Kwenda Kuuza Kwa Bei Ya Jumla Dar. Nimeanza Ruaha Mbuyuni, Nitaenda Singida Na Hata Ilula Iringa Na Sehemu Zinginezo. Nimejipanga Kwa Atleast Kila Wiki Niingize Mzigo Dar Kama Nitapata Network Nzuri. Kama Kuna Uwezekano Unaomba Nisaidie Kujenga Network
 
Mia mia,kila la kheri mkuu ktk biashara.Zingatia uaminifu,uadilifu na uvumilivu,ni muhimu ktk biashara,bila kusahau kutafuta taarifa rasmi za masoko kwa wakati husika,sio stori za mwezi uliopita,unakurupuka na mzigo kumbe bei imeshuka,chalii.
 
Nashukuru Sana Ndugu. Nimekuwa Nikiangaika Kutafuta Wateja Bado Sijafanikisha Sana Hadi Sasa Nimempata Mmoja. Je Kama Unaweza Kuniunganisha Na Wateja Ikiwa Unawafahamu Nitafurahi Zaidi.
dada, shkamoo, mimi nipo dar. nimetumia jamii form nimepata wateja wa sungura. nitakutafutia wateja kwa kadri ya uwezo wangu lakini naomba uni pm nipate namba yako nahitaji unipe maelezo kuhusu maeneo ya kufanya kilimo hiki mwakani ninaweza kujiunga na ujasiliamal wa kilimo hiki
 
Asante Mkuu Kwa Ukarimu Wako. Aina Za Vitunguu Red Creoles Ambovyo ni Vikubwa2 Na Size Ya Kati. Ninagunia 90 Kutoka Ruaha Mbuyuni. Mimi Silimi Bali Naingia Kwenye Business Hii Kwa Mara Ya Kwanza Kwa Kukusanya Kutoka Kwa Wakulima Na Kwenda Kuuza Kwa Bei Ya Jumla Dar. Nimeanza Ruaha Mbuyuni, Nitaenda Singida Na Hata Ilula Iringa Na Sehemu Zinginezo. Nimejipanga Kwa Atleast Kila Wiki Niingize Mzigo Dar Kama Nitapata Network Nzuri. Kama Kuna Uwezekano Unaomba Nisaidie Kujenga Network

Wewe hao wakulima wanakupangia bei ama wewe ndo unawapangia ? Maana nilikuwa huko nao walikuwa na kilio hicho hicho kuwa wachuuzi toka mjini wanawapunja sana
 
Kweli kilimo cha kitunguu ni kizuri na mkomboz mkubwa. Binafsi nafanya biashara ya vitunguu kwa kulima na kununua kwa wakulima pia, ko kwa mwezi naingiza fuso tatu za gunia 90 (90*3=180). Soko langu kuu ni kkoo na hiyo ni kutokana na kwamba wafanya biashara wengi ni waoga kununua mzigo moja kwa moja toka kwa mfanyabishara na wanaamua kununua toka kwa dalali kwasababu wanakua safe incase bidhaa ikiwa sio nzuri wanarejesha. Kweli biashara ya kutua kariakoo mzigo ni kikwazo sana kwasababu sometimes unaweza kutana na bei nzur au bei ya kawaida lakin siku zote bei za kkoo zinategemea na bei za mzigoo shambani. Pia ili kupata faida wateja wengi wanaangaalia vitunguu vimetokea mkoa gan kwasababu kila mkoa vitunguu vyake vina bei tofauti. Ushauri wangu ni huu:
Tafuta wateja wako wa direct ambao utakua na uhakika wa kuwashushia gunia 20 hata kwa kila mzigo unaoleta mjini, ila pia peleka kkoo kwasbabu lile ndo soko kuu na kutokana na mfumo wa kibiashara uliotengenezwa ni lazima ukauzie katika masoko makubwa ili uweze kupiga hatua.
Nakwambia haya kwasababu me nafanya hii biashara na huu ni mwaka wa tatu na imeleta mabadiliko makubwa sana ndan ya maisha yangu. Kuwa makini tu na madalali matapeli. Ahsante

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Unawezaje kubaini madalali matapeli?
 
Shukrani nyingi kwa baraka607, japo ni taarifa za biashara hususani soko kuchukuliwa kama sehemu nyeti ya biashara, hapo ndio wakulima tunapoumizwa, tunahitaji kuziweka wazi na kufanya mageuzi ya soko "kupunguza nguvu ya dalali" hapo ndipo jasho la mkulima litakapopanda thamani.
n.b. Kwa macho ya dalali mkulima na mfanyabiashara wa jumla wote ni wakulima.
Kweli kilimo cha kitunguu ni kizuri na mkomboz mkubwa. Binafsi nafanya biashara ya vitunguu kwa kulima na kununua kwa wakulima pia, Soko langu kuu ni kkoo, kwa Kweli biashara ya kutua kariakoo mzigo ni kikwazo sana kwasababu sometimes unaweza kutana na bei nzur au bei ya kawaida lakin siku zote bei za kkoo zinategemea na bei za mzigoo shambani. Pia ili kupata faida wateja wengi wanaangaalia vitunguu vimetokea mkoa gan kwasababu kila mkoa vitunguu vyake vina bei tofauti. Ushauri wangu ni huu:
Tafuta wateja wako wa direct ambao utakua na uhakika wa kuwashushia gunia 20 hata kwa kila mzigo unaoleta mjini, ila pia peleka kkoo kwasbabu lile ndo soko kuu na kutokana na mfumo wa kibiashara uliotengenezwa ni lazima ukauzie katika masoko makubwa ili uweze kupiga hatua.
Kuwa makini tu na madalali matapeli. Ahsante
 
Nashukuru Sana Je Unaweza Niunganisha Na Baadhi Ya Wanunuaji Wa Jumla Unaowafahamu Ndugu? Iwe Soko La Kkoo Au Lolote Lile Namba Yangu Ni 0684061951
 
Nashukuru Sana! ni vitunguu vya mkoa gani vinalipa? Je Unaweza Niunganisha Na Baadhi Ya Wanunuaji Wa Jumla Unaowafahamu Ndugu? Iwe Soko La Kkoo Au Lolote Lile Namba Yangu Ni 0684061951
 
Unawezaje kubaini madalali matapeli?

Fanya research, pale kkoo kuna madalali ambao wako pale miaka 10 na zaidi, kwahiyo hao ndo watu wa kudeal nao manake ile ndo ajira yao na hawawezi kuondoka kkoo labda itokee amekufa. Ko kabla hujaleta mzigo katafute madalali angalau wawili pale kkoo na ilala upate mmoja, hiyo itakuwezesha kumaliza mzigo wako haraka na kupata pesa yako haraka.
 
Nashukuru Sana Je Unaweza Niunganisha Na Baadhi Ya Wanunuaji Wa Jumla Unaowafahamu Ndugu? Iwe Soko La Kkoo Au Lolote Lile Namba Yangu Ni 0684061951

Me bwana kukuunganisha ni ngumu kwasababu siku yakikukuta ya kukuta itakua kama me nimekuingiza kwenye mtego wa panya, manake dalali anaweza kuwa mzuri kwangu ila kwako akawa mzinguaji. Nenda kkoo ulizia kibaga na ilala ulizia mzee mgotto. Ndo madalali wakubwa. Ila wewe pia fanya research yako kabla hujawaletea mzigo.
 
Back
Top Bottom