Vituo gani vya mafuta vinauza super unleaded petrol hapa Tanzania

Vituo gani vya mafuta vinauza super unleaded petrol hapa Tanzania

RJ45

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2014
Posts
340
Reaction score
117
habari zenu wakuu!

nimekuwa nikifuatilia mjadala wa tofauti kati ya unleaded petrol na super/premium unleaded petrol nikagundua super unleaded ni nzuri kutumia kwa gari yoyote huku ikiwa na faida nyingi. naomba kufahamishwa kwa hapa tanzania ni kampuni gani au vituo vya mafuta vinauza hii super unleaded petrol.

nawasilisha
 
Mkuu mimi sijajua exactly ni vituo gani vinauza Premium. Ingawa baadhi ya vituo vya mafuta huwa wanakuwa wameandika wanauza premium. Nadhani mfano ni total kama sijakosea.

Ila ninachoweza kusema ni kwamba, kama gari yako wamerecommend utumie premium weka premium kama wameshauri uweke unleaded weka unleaded. Hakuna tatizo lolote.

Kabla ya manufacturers kutoa hizi recommendations huwa wanafanya testing ya haya mafuta. Then ndio wanarecommend.

Na ndio maana si kila manufacturer karecommend premium.

Mwisho hakuna manufacturer ambaye angetaka final consumer wake atumie mafuta mabaya.
 
Mkuu mimi sijajua exactly ni vituo gani vinauza Premium. Ingawa baadhi ya vituo vya mafuta huwa wanakuwa wameandika wanauza premium. Nadhani mfano ni total kama sijakosea...
kwa research ndogo nliofanya kila gari inafaa na wanashauri kutumia premium lakini sio kila gari inafaa kutumia unleaded. maana yake gari ambayo manufacturer ameshauri utumie unleaded ukitumia premium ni bora zaidi lakini gari ambayo wanarecommend premium unleaded ukitumia regular unleaded ni tatizox
 
Okay,

Maneno yangu ya mwisho naweza kusema kwamba Premium fuels zimetengenezwa kwa ajili ya performance engines. Zina Octane number kubwa ambayo inaact kama resistance towards engine knocking. Kama una performance engine, mfano sport cars and the likes basi weka premium.

Ila kama una gari ya kawaida basi weka tu unleaded sababu hakutakuwa na utofauti wowote na atakayeweka premium. Zaidizaidi tu aliyeweka premium atatingia gharama kubwa.
 
habari zenu wakuu!

nimekuwa nikifuatilia mjadala wa tofauti kati ya unleaded petrol na super/premium unleaded petrol nikagundua super unleaded ni nzuri kutumia kwa gari yoyote huku ikiwa na faida nyingi. naomba kufahamishwa kwa hapa tanzania ni kampuni gani au vituo vya mafuta vinauza hii super unleaded petrol.

nawasilisha
Mimi sio Mtaalamu wa fuels lakini kwa Tanzania, mafuta yanayoingoza ni ya vituo vya Total, mafuta yao ni Total Exellium, yanafutiwa na vituo vya Puma wao wana unleaded na Engen wao wana premium.

Kuhusu mafuta ya Total, karibu mitaa hii

Phttps://www.jamiiforums.com/threads/jee-kuna-ukweli-kuwa-in-tanzania-mafuta-ya-vituo-vya-total-they-are-the-best-if-yes-how-wakati-tunanunua-bulk.1550460/

P
 
Sidhani kama Kuna mafuta yenye lead Siku hizi, lead ilipigwa Vita sana , however Kila blender anajitahidi kuweka additives anazozijua ili kuboresha mafuta yake, Total kwa mfano Wana exellium sijui ni kitu gani hasa Ila Wana claim huwa kinongeza efficiency , what is strange to me ni kuwa ipo kwenye diesel na petrol zao,
 
Back
Top Bottom