Vituo vya afya 234 mwiba mchungu

Vituo vya afya 234 mwiba mchungu

Misa ya pili

Member
Joined
Mar 24, 2023
Posts
85
Reaction score
170
Miaka 2 iliyopita baada ya kuapishwa Rais Samia, TAMISEMI chini ya Bashungwa walianzisha ujenzi vya vituo vya afya na zahanati kila kijiji na pesa kupelekwa katika kila halmahsauri vikitakiwa vianze kutumika kabla ya mwezi wa 11, 2022 lakini mpaka sasa ni mwiba mchumngu.

Halmashauri nyingi miradi imesimama na pesa zimekwisha mil 500 kwa vituo vya afya, na cha ajabu zaidi watumishi walishapangiwa vituoni tangu mwezi wa 7, 2022. TAMISEMI chini ya Waziri Kairuki hili mkaliangalie vipaumbele vya halmashauri ni vipi kama sio afya na elimu.
 
Hiyo sio tu kwenye zahanati, hadi hospital za halmashauri ndio mambo hayo hayo watu wanakula mishahara na kazi hakuna.. wakurugenzi wanafungua hospital hazina baadhi ya vitu muhimu... Kifupi walikurupuka hela zimekata na kazi hazijaisha, nchi yangu huzuni sana.
 
huzuni kubwa sana ,badala ya kujenga kwa mkupuo kwanini wasichangue baadhi ya halmashauri zenye uhitaji mkubwa na ujenzi ukawa chini ya wizara za afya kuliko kuwaachia hizi halmashauri zetu zilizojaa machangamoto ya upigaji
 
Kwahiyo unataka kuniambia mwaka huu watu wa afya wasahau kuhusu kuajiriwa? Maana kwa maelezo Yako inavyoonekana Kuna akiba ya kutosha ya watumishi wa afya kwasasa.
 
sidhani kama anamaana hiyo swala la upungufu wa watumishi kwenye afya na elimu alijawai kutosha TZ kikubwa kuonesha ukubwa wa tatizo la kushindwa kukamilika kwa miradi ya afya katika halmashauri nyingi mpaka watumishi kukosa kazi kwakua hata hizo theater kwa ajiri operation bado azijakamilika na mengineyo
 
Kwahiyo unataka kuniambia mwaka huu watu wa afya wasahau kuhusu kuajiriwa? Maana kwa maelezo Yako inavyoonekana Kuna akiba ya kutosha ya watumishi wa afya kwasasa.
Hapana watumishi hawatoshi kabisa mkuu.. isipokuwa miondombinu bado haijakaa vizuri sehemu kubwa sana... Mfano kuna halmashauri ziliomba watumishi wa afya katika hospital za wilaya 200+ ila wamepewa 70+....
 
Hospitali, vituo vya afya, zahanati inatakiwa kujengwa kutokana na uhitaji kwa kuzingatia utaalamu.
Kuna maeneo yenye magonjwa na uhitaji kuliko mengine.
Hata hivyo, kwa sababu ya siasa zetu za kukariri, vituo vingi vitajengwa bila kuzingatia idadi ya watu, takwimu za magonjwa na jiografia za maeneo husika.
 
huzuni kubwa sana ,badala ya kujenga kwa mkupuo kwanini wasichangue baadhi ya halmashauri zenye uhitaji mkubwa na ujenzi ukawa chini ya wizara za afya kuliko kuwaachia hizi halmashauri zetu zilizojaa machangamoto ya upigaji
Mfano kweli wangeangalia sehemu zenye uhitaji mkubwa mfano wilaya ya hai Kuna vituo vya afya karibu alafu wanaanzisha vituo vipya vya Nini na mahitaji siyo makubwa mfano Kuna kituo Cha afya masama na kirani vimeoishana urefu wa kilometa mbili kwenye kata Moja na kutoka kutoka kituo Cha masama wameanzisha kituo kingine Cha lemira umbali vimepishana kilometa Tano na kutoka hicho Lemira Kuna kituo Cha nkwansira ukiangalia upana na urefu wa hivyo vituo vyote vinne hakuna umbali wa kilometa Saba wakati Kuna kata yenye urefu wa kilometa 40 kituo kimoja yaani kutoka Kijiji Hadi kwenye kituo Cha afya mama mjauzito anatembe kilometa 20
 
Mkuu Ni kweli kabisa kwa ramani ya hapo Hai unaijua vyema
 
Hii ndio tatizo lililopo baadhi ya vituo vimerundikwa sehemu moja hadi watumishi wanakosa wa kuwahudumia na kwingine hakuna hata kimoja sijui vigezo gani viltumika.Wakati mwingine siasa zinaathiri sana maendeleo.
 
Nadhani na baadhi ya zahanati zinapelekewa fedha ndogo kuliko uhitaji wake mfano hizi ramani wameleta bila kuzingatia eneo unakuta zahanati imejengwa kwenye kijiji chenye kaya 200 ila inaukubwa kama hospital alafu inapewa mil 50 ya kufanyia finish
 
Back
Top Bottom