Vituo vya Afya Vitano Vipya Vyajengwa Wilaya ya Hai

Vituo vya Afya Vitano Vipya Vyajengwa Wilaya ya Hai

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

VITUO VYA AFYA VITANO VIPYA VYAJENGWA WILAYA YA HAI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kusogeza huduma za Afya karibu na wananchi kwa kujenga vituo vya Afya Vitano katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro.

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amesema hayo Oktoba 4, 2024 akiwa katika ziara ya siku Sita Mkoani Kilimanjaro ambao ameanza kwa kukagua na kuzindua miradi ya Sekta mbalimbali iliyotolewa fedha na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwemo Sekta ya Afya.

"Mkoa huu wa Kilimanjaro umepokea zaidi ya Bilioni 10 ili kutekeleza miradi ya Afya vilevile Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongeza milioni 150 kwa ajiri ya vifaa tiba vitakavyotumika katika kituo cha Afya Masama Kati." Amesema Waziri Mhagama

Aidha, Waziri Mhagama ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai pamoja na Mganga Mkuu wa Mkoa kukamilisha ununuzi wa vifaa tiba ili Zahanati ya Kimashuku ianze kufanya kazi ifikapo Oktoba 30 mwaka huu.

"Kwa kuwa Mhe. Rais Samia ameleta Milioni 100 ya umaliziaji wa Zahanati hii na Milioni 50 ya ununuzi wa vifaa tiba, jambo la kwanza naomba fedha ya vifaa ipelekwe Bohari ya Dawa haraka sana, nimachotaka kuona Zahanati hii upatikanaji wa dawa usiwe wa mashaka." Amesema Waziri Mhagama

Waziri Mhagama ameukata uongozi huo kuhakikisha huduma za uzazi wa dharula kwa kina mama zinapatikana ikiwemo vitanda maalum vya kujifungulia ili wakina mama wapate eneo salama na zuri la kujifungua na kuwapunguzia adha wananchi ya kufuata huduma hizo mbali.

"Tunatamani Zahanati hii iwe mkombozi kwa akina mama, wazee, vijana na watoto wetu, nitoe wito kwa Halmashauri yetu kuhakikisha Zahanati yetu inasimamiwa vizuri na tunaamini Zahanati hii itaenda kutoa huduma zinzotakiwa." Amesisitiza Waziri Mhagama

Mwisho, Waziri Mhagama amewataka wananchi wote wa Hai kwenda kujiandikisha kuboresha taariza kwenye tume ya uchaguzi ili kupata fursa ya kuwachagua viongozi wa Serikali za mitaa ambao wanaleta maendelea katika maeneo yao.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2024-10-04 at 21.06.44.mp4
    6.3 MB
  • GZEP2ahX0AAoShG.jpg
    GZEP2ahX0AAoShG.jpg
    158.3 KB · Views: 5
  • GZDrU9jXAAA025e.jpg
    GZDrU9jXAAA025e.jpg
    320.3 KB · Views: 5
  • GZDrU9jWgAAA7FI.jpg
    GZDrU9jWgAAA7FI.jpg
    366.5 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-10-04 at 21.06.51.jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-04 at 21.06.51.jpeg
    203.6 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-10-04 at 21.06.50.jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-04 at 21.06.50.jpeg
    248.7 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-10-04 at 21.05.50.jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-04 at 21.05.50.jpeg
    177.1 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-10-04 at 21.05.49.jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-04 at 21.05.49.jpeg
    150.3 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-10-04 at 21.05.48.jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-04 at 21.05.48.jpeg
    218.3 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-10-04 at 21.05.45.jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-04 at 21.05.45.jpeg
    263.5 KB · Views: 4
I lazima make go takamilike kabla ya uchaguzi, yatatuongezea kura. Kazı iendelee.
 
Back
Top Bottom