SoC04 Vituo vya huduma jumuishi ni mwarobaini tatuzi wa kero za wananchi (One Stop Service Center)

SoC04 Vituo vya huduma jumuishi ni mwarobaini tatuzi wa kero za wananchi (One Stop Service Center)

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Apr 20, 2024
Posts
25
Reaction score
26

Chanzo: safari Media
Chanzo: Safari Media
VITUO VYA HUDUMA JUMUISHI.
Ni namna ya kusogeza huduma karibu na wananchi.
Ni mjumuiko wa taasisi/mashirika ya kiserikali na binafsi katika eneo moja ili kutoa huduma kwa jamanii/wananchi. Mfano BRELLA, WCF, MANISPAA/HALMASHAURI, NIDA, TRA, NSSF, RITA, HESLB, IMMIGRATION, Taasisi za kifedha (NMB, BOT, CRDB & NBC), Mitandao ya simu (TIGO, VODACOM & AIRTEL). Hii yote ni katika kuboresha huduma za kijamii na kupunguza msongamano na kero/malalamiko ya wananchi katika taasisi/kampuni husika.

"Kupima utendaji wa kiongozi yoyote inahitaji kuangalia namna anavyoweza kutatua changamoto za watu anaowaongoza. Uwepo wa kero/malalamiko ni ishara ya udhaifu katika uongozi"

"Kama nchi tunatamani kufika mbali, inatupasa kukimbizana na wakati katika utendaji na kushughulikia malalamiko/kero za wananchi haraka na mapema ila kuepuka upotefu mapato"

Hali ya sasa ya utolewaji wa huduma na taasisi za kiserikali/Binafsi.
1. Kumekuwa na kero/malalamiko sana juu ya taasisi/mashirika ya kiserikali na binafsi, kutokana na huduma mbovu, tunaweza kuona dhahiri katika mikutano ya viongozi jinsi watu wanavyoshikilia mabango ya malalamiko/kero. Mfano tunaweza kuona katika mikutano ya mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paulo Makonda na Waziri wa Ardhi Mh. Jerry Silaha.

2. Msululu/Msongamano wa watu katika taasisi za kiserikali ili kupata huduma, Mfano. Ukifika katika ofisi za Ardhi, NIDA, TRA na HALMASHAURI/MANISPAA, Utakutana na foleni ambayo inakatisha tamaa na wengi hushindwa kupata huduma kulingana na foleni au kupewa huduma ya kiwango cha chini.
3. Mlundikano wa kazi/files. Kumekuwa na kazi nyingi kiasi kwamba watendaji husika kushindwa kuzitatua kwa wakati na hii inapelekea ucheleweshwaji wa huduma na upotevu wa haki za wananchi.
4. Mizunguko/Kuzungushwa katika taasisi kadhaa wa kadhaa ili kupata huduma fulani. Mfano, unahitaji TIN Number, inakuhitaji uwe na Kitambulisho cha taifa na itakuhitaji uende kwanza NIDA halafu baadae urudi TRA.

Swali la kujiuliza, Masanduku ya Maoni yaliyopo katika Taasisi husika, Tovuti/Application ya e-MREJESHO na namba ya msimbo kupokea malalamiko *152*00# na Viongozi husika wa maeneo, Wanashindwa vipi kutatua na kumaliza malalamiko/Kero za wananchi??
Ni swali ambalo linafikirisha sana na linaonyesha udhaifu mkubwa kwa namna moja au nyingine na linaleta picha hii;-
1. Wahusika katika taasisi husika, hawatilii maanani maoni yanayotolewa na wananchi kwa maslahi yao binafsi.

2. Kutokuwepo kwa idara fuatiliaji na tekelezaji kero za wananchi, huenda sanduku za maoni zipo ila hakuna idara maalumu ya kushughulikia hayo maoni, hata kama idara ipo basi hakuna watekelezaji yaani watu wanao hakikisha maoni yaliyopokelewa yanafanyiwa kazi ipasavyo.

3. Watu katika mamlaka za kiserikali wamelizika kiasi kwamba wanasubiri mishahara tu, bila kuwajibika ipasavyo, kuna haja ya kuwa na tathimini ya utendaji katika Mamlaka za kiserikali na kutumia mifumo iliyopo kama PEPMIS, PIPMIS na HR ASSESSMENT.

WhatsApp Image 2024-06-06 at 4.11.29 PM.jpeg

chanzo: Kitini cha Serikali.

4. Katika mamlaka za kiserikali kuna tabia ya kufichana uovu/kuogopana na kulindana, Ujamaa na undugu maofosini kiasi kwamba kila mtu ana mtu wake. Kitu ambacho kina dhoofisha na kuchafua sifa na taswira ya taasisi za serikali, kwenda kuathiri nchi na kudidimiza uchumi.

3. Hakuna mamlaka wajibishaji katika taasisi husika, ambazo zinahakikisha uzembe wowote unaojitokeza basi mhusika anawajibishwa ipasavyo.

Mapendekezo kwa Serikali, Mashirika Binafsi na Wananchi.
A. Kwa Serikali.
1. Serikali iweke vituo vya huduma jumuishi kila wilaya. Vituo hivi vya huduma jumuishi vitakuwa kila wilaya, sehemu ambayo ni katikati ya mji ili kuwezesha wananchi kufika na kupata huduma zote kwa pamoja.

2. Kila taasisi/shirika la kiserikali lazima lijumuike katika kituo cha huduma na kutoa huduma stahiki ili kuwezesha na kuharakisha utoaji huduma.

3. Huduma ya vituo jumuishi kufanyika walau mara moja kwa mwezi ili kupunguza, kutatua kero na uharakishwaji wa huduma kwa wananchi. kwani inajengwa taifa linalowajibika na kufanya kazi Kwa bidii ili kujenga Uchumi imara.

B. Kwa Taasisi/Kampuni Binafsi.
1. Kampuni/Taasisi binafsi zinaweza kuwa na utaratibu wa vituo jumuishi kwa namna yao wenyewe au kuungana na serikali katika huduma jumuishi ili kuhakikisha huduma inafikia wateja kwa wakati.

2.- Ni wakati sahihi kwa kampuni/taasisi binafsi kujitangaza kwa jamii katika kuboresha huduma zao.

C. Kwa Wananchi.
1.- Hii ni fursa ya taifa kukua kiuchumi, uwepo wa vituo jumuishi unaenda kuweka kasi ya utendaji kazi Kwa utatuzi wa kero za wananchi kwa wakati na kuunganisha kati ya wananchi na watendaji wa serikali na kutoa matabaka.

2. Kujitokeza kwa wingi na kuhakikisha wanapata huduma stahiki, kwani vituo hivi vinakuja kwa ajili ya wananchi.

Tujikumbushe kutoka kwa Mh. Godwini Gondwe na "
One Stop- JAWABU"
Mwaka 2020, Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Temeke Mh. Godwin Gondwe, alianzisha "ONE STOP JAWABU" na ilizunguka wilaya mbili (TEMEKE & KINONDONI) na ilileta matokeo yafuatayo;-
  1. Ilileta taswira ya taifa linalojalia na kuweka kipaumbele cha wananchi wake kwa kutatua changamoto zao kwa urahisi na wakati.
  2. Mwitikio wa wananchi wengi walijitokeza ili kupata huduma mbalimbali.
  3. Furaha na kuridhishwa juu ya kituo cha huduma jumuishi.

View: https://www.youtube.com/watch?v=Ncssz6Df3qQ

WhatsApp Image 2024-06-06 at 3.15.05 PM.jpeg

Chanzo: tovuti ya H/Manispaa ya kinondoni
Uwepo wa kituo cha huduma jumuishi utaleta matokeo yafuatayo.
  1. Kupunguza kama sio kuondoa kabisa kero na malalamiko ya wananchi kwa uongozi na kuongeza upendo na uaminifu kwa viongozi.
  2. Hatutoona Mabango makubwa yanayoelezea kero/malalamiko fulani katika mikutano ya viongozi.
  3. Tutaweza kuokoa mapato mengi ambayo tulikuwa tunayapoteza kwa ucheleweshwaji wa huduma.
  4. Taifa lenye wananchi walio na furaha, Upendo na uaminifu kwa viongozi.
  5. Inaondoa matabaka katika ya wananchi na watendaji wa serikali na kulileta taifa pamoja.
  6. Inajenga taifa lenye kuwajibika na kujadi zaidi masilahi ya watu wake katika kupiga hatua zaidi katika nyanja zote.
MWISHO
Tanzania ni nchi nzuri sana na yenye fursa nyingi, Mungu ametubariki sana, Tunachohitaji ni viongozi. WAAMINIFU, WAADILIFU, WATIIFU. JASIRI. WENYE MAONO & KULIPENDA KWA DHATI TAIFA LA TANZANIA.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom