Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Jeshi la Wananchi wa Tanzania ni jeshi la sita kwa ubora duniani.
Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa, duaniani kuna nchi 195.
Katika nchi zote hizo, jeshi la Tanzania ni la 6 kwa ubora. Maana yake ni kwamba Tanzania imezipita nchi 189 kwenye ubora wa kijeshi.
Hakika Tanzania iko juu sana. Ubora huo wa jeshi letu huthibitishwa na maonyesho ambayo huonyeshwa na makomandoo wetu kwenye sherehe mbalimbali za kimataifa.
Sasa, huwezi tu kuwa jeshi bora hivi hivi bila kuwa na chochote.
Juzi juzi hapa China imefanya majaribio ya ndege ya kijeshi inayosadikiwa kuwa ni ya kizazi cha 6 [6th generation].
Kwa sasa, ni nchi tatu tu zilizo na mchakato wa kutengeneza hizo ndege. Ni USA, Russia, na China.
Jeshi letu lililo la sita kwa ubora, lina hata 5th generation fighter jet hata mbili?
Majeshi karibu yote yaliyo bora yana vituo vya kijeshi vilivyopo kwenye nchi zingine.
JWTZ ina overseas military bases ngapi na ziko wapi?
Huwezi kabisa kuwa na jeshi la 6 kwa ubora halafu ukose hivyo vitu viwili.
Vya JWTZ viko wapi?