LGE2024 Vituo vya kuandikisha wapiga kura vyageuka vijiwe vya kupigia soga

LGE2024 Vituo vya kuandikisha wapiga kura vyageuka vijiwe vya kupigia soga

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mwanongwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2023
Posts
611
Reaction score
567
Kama mwenendo wa kujiandikisha Kwenye daftari la mkazi kwaajili ya kupiga kura Kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unasua sua hivi,vipi uchaguzi mkuu mwakani?

Wananchi wengi katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Mbeya nikama wamesusia zoezi hili la kujiandikisha wakidai ni kupoteza muda wao tu.

Huku makalani wanaoandikisha wakiwa muda mwingi wanapiga soga tu kutokana na uchache wa wananchi wanaojitokeza.

Story zilizopo mitaani ni kwamba kile ambacho kilitokea wakati wa uchaguzi kama huu wa serikali za mitaa mwaka 2019 Cha wagombea wa chama kimoja kupita maeneo mengi bila kupingwa ndiyo sababu ya wananchi kutojitokeza kwa wingi kujiandikisha.

Leo nimepita Kwenye baadhi ya mitaa na kujionea hali ilivyo,licha ya hamasa kubwa ya viongozi wa vyama na serikali kuhamasisha lakini hali ni Tete.

Soma Pia: Special Thread: Hali ya Vituo vya Kujiandikisha kupiga Kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 kwa Picha na Video

Mitaa kama Ivumwe,Mwakibete,Ntundu,Itezi,Iduda,Tonya,Ituha na mingine mingi, Makalani Wanapiga soga tu huku wengine wakiwa wanauchapa usingizi.

Wananchi wanasema vyovyote itakavyokuwa kwao ni sawa tu lakini kwenda kujiandikisha ni kupoteza muda wao
Vituo vingi vimekuwa havina idadi kubwa ya wananchi ambao wanajiandikisha.

Wananchi wenzangu tujitokeze Kwa wingi kujiandikisha ili tuitumie haki yetu ya msingi ya kuchagua viongozi tunaowataka watuongoze Kwa kipindi Cha miaka mitano ijayo
 
Kuna karani mmoja alichukua namba angu wakati najiandikisha

Nashangaa yupo busy online na mie muda wote hadi najiuliza hiyo kazi anafanya muda gani
Wananchi wamesusia zoezi kabisa
 
Kuna karani mmoja alichukua namba angu wakati najiandikisha

Nashangaa yupo busy online na mie muda wote hadi najiuliza hiyo kazi anafanya muda gani
Muda mwingi wanakuwa wamelala tu
 
Kuna karani mmoja alichukua namba angu wakati najiandikisha

Nashangaa yupo busy online na mie muda wote hadi najiuliza hiyo kazi anafanya muda gani
Akishachukua namba Yako ujue umeshachagua kijani upende usipende
 
Kuna karani mmoja alichukua namba angu wakati najiandikisha

Nashangaa yupo busy online na mie muda wote hadi najiuliza hiyo kazi anafanya muda gani
Hahahahah kumbe ni wewe.. sasa nini kutusimanga. Raia wenyewe wanasubiria kesho ndo waje.
 
Back
Top Bottom