Hivi vituo vya kupigia kura vinatakiwa vifungwe saa ngapi? Nimesikia katika TV channel moja kwamba vinafungwa saa 10.00 jioni. Kwa maoni yangu ni mapema mno na sioni sababu yoyote kwanini visifungwe saa 12.00 jioni.
ni saa kumi ndio. Huo ndo utaratibu uliowekwa toka mwanzo na sidhani kuna uwezekano wa kubadili hilo.
Atakayekuwepo kituoni kwa muda huo atapiga kura lakini atakayekuja baada ya hapo ple zake, atakuta njagu kasima nyuma ya mtu wa mwisho.
Mie nimepiga mapema kabisa ila kwa idadi ya wapiga kura 19 millioni na wengine hawajaona majina yao hadi saa hizi pamoja na kuwa walifika mapema kabisa vituoni kwao, kufunga vituo hivyo saa 10.00 jioni naona si sawa kabisa.