JAYJAY
JF-Expert Member
- Oct 31, 2008
- 8,191
- 8,490
Wadau, nimeshaona minara yakurushia matangazo ya redio mara nyingi kila kituo kina minara yake (sijui kama kuna vituo vina'share' matumizi ya minara hiyo).nimewahi kusoma kuwa katika mfumo wa digital vituo havitakuwa na kazi ya kurusha matangazo bali kuna kampuni zimepewa kazi hiyo(nadhani ni 'multiplexor' kama sijakosea). je, wadau hii inamaanisha kuwa hizo kampuni ndizo zitakuwa au zitatakiwa kumiliki au kuweka minara hiyo?, je hii inamaanisha pia kuwa mchakato wa kufungua au kuanzisha redio utakuwa nafuu kwa sababu mmiliki hatatakiwa tena kufikiria gharama za uwekezaji kwenye minara au kutakuwa na gharama zitakazochajiwa na hizo kampuni? je, gharama hizo hazitaweza kuwa kikwazo kwa uanzishwaji wa redio? vipi pia kuhusiana na vituo vya tv, je mchakato ni huo huo kama wa redio?