benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Serikali kupitia Shirika la Wakala wa Meli nchini (TASAC), imeeleza kuwa inatarajia kujenga vituo vya uokoaji katika Maziwa Makuu nchini ili kusaidia katika tahadhari na uokoaji pindi yanapotokea majanga kwenye vyombo vya usafiri wa majini.
Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC, Kapteni Musa Hamza Mandia akizungumza baada ya kukagua shughuli za TASAC mkoani Kigoma, , amesema kupitia ilani ya CCM, TASAC imeelekezwa kujenga vituo vya uokoaji na kwamba tayari wameainisha maeneo ambayo vituo hivyo vitajengwa huku mchakato wa kupata mzabuni wa boti za kisasa za uokoaji nao ukiendelea.