fakhbros
JF-Expert Member
- Sep 14, 2013
- 384
- 658
Kuna aina maalum na ya kipekee ya watu ambao hawapendi kwenda nje na wanapendelea kukaa kwenye vyumba vyao tu,
Wanapoenda mahali fulani, hukosa upweke wao wenye kupendeza.
Hawa ni watu ambao wana rafiki mmoja au wawili wa karibu na hawaingiliani na mtu mwingine yeyote katika maisha yao.
Hawa ni watu wale wale ambao simu zao ziko kimya kila wakati huwezi kuwaona wakipiga au kupokea,
Na hawamuongelei mtu yeyote wao hujiongelea wenyewe,
badala yake, wao huchanganyikiwa mtu anapowauliza jambo fulani linalowahusu wao au watu wengine, huwa ni watu wasiokuwa na taarifa juu ya wengine,
kuzungumza nao, au kujaribu kujumuika nao ni jambo linalo hitaji uangalifu zaidi sababu hawa sio watu wanao shoboka kwenye mambo ya watu,
Hao ndio wanaofungua Jamii forums kila siku bila kupost chochote au kuchangia hoja yoyote ile wanayo kutana nayo, wanaweza kusoma na kusonya kama hoja hawajaelewa na wakacheka kwa tabasamu kama wameelewa somo,
Hawa watu wanaishi katika hisia zao wenyewe,
na hawa ni watu wanaopenda kusoma vitabu, kutembelea fukwe za bahari, kucheza kwenye mbuga au jangwa, na kupanda Milima kama Kilimanjaro,
hufurahia hali ya hewa yenye baridi, wanatabia za samaki kiasi furani kuishi kwenye Jokofu wakiwa hai,
na moioyo yao ina amani kila wakati.
Giza na upweke vinawapa kilevi kwao.
hawa ndio wale ambao swala la Ndoa kwao limebaki kuwa ni kharamu hata wakiingia katika ndoa huwa hawadumu na wapenzi wao ni watu wanao hitaji utulivu wa kipekee katika nyakati zote,
Hawa ndio wale ambao hutabasamu kila wakati, hawajui neno kununa kwenye maisha yao, wanapo kuwa na hasira huongea kwa Ishara hawajui kuinua mikono yao kwenye kutoa adhabu,
Hawa ndio wana wapotevu katika mawazo yao, hawamdhuru mtu yeyote kwenye maamuzi yao,
Ukiwa na watu wa aina hii kwenye mahusiano tegemea kupata kila kitu utakacho kihitaji kutoka kwao ila hawachelewi kukuepuka ikiwa watagundua kuwa wewe ni katika wale wala Mizoga,
Hawa ni waumini wazuri wa vitu vya kusadikika wao hutafuta ukweli kwa njia ya Maandishi,
Na hawa sio viongozi wazuri katika kila idara sababu uongozi ni jambo la kujitoa sadaka kwa wengine lakini hawa ni watu wabinafsi wanajari zaidi mambo yao,