Viungo vipi vya chakula ungependa kuvipata vikiwa vimefungashwa?

Viungo vipi vya chakula ungependa kuvipata vikiwa vimefungashwa?

mr gentleman

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,222
Reaction score
4,689
Habari zenu wadau wa maakuli?


Mimi nilikuwa napenda kufahamu ungependa upate viungo gani vya chakula ambavyo vimeshaandalliwa na kufungashwa ili kurahisisha mapishi yako....


Nawakaribisha nyote mnipe mawazo yenu ninategemea kuanza kupakia viungo katika package za kisasa ili ziuzwe kwenye maduka na masoko yanayoweza kufikiwa na watu wa madaraja yote nikianzia nyumbani baadae nje ya nchi.
 
Tandoor masala ina spice zote unaweza pikia kuku,pilau na mchuzi....

Na kuna tea masala pia safi sana unaweza pata huko au zanzibar ila ntakutumia picha ujipatie na wewe
 
Mimi natamani kila kiungo kinachopatikana hapa kwetu kifungashwe.Maana kiungo kikifungashwa kinaongezeka thamani.
 
Tandoor masala ina spice zote unaweza pikia kuku,pilau na mchuzi....

Na kuna tea masala pia safi sana unaweza pata huko au zanzibar ila ntakutumia picha ujipatie na wewe

farkhina nadhani haujanipata dadangu...Mimi ndio nataka kufungasha hivyo viungo kisha niuze mfano nimefikiria kupakia viungo vya pilau, kuna yale majani ya chai watu wanayapenda wanaita michai chai, hiriki, tangawizi tunataka tuvifungashe kisasa zaidi.

So nilitaka mawazo na mapendekezo zaidi toka kwenu wadau wa jikoni .
 
Last edited by a moderator:
Nitajie viwili vitatu basi mkuu.
Hapo kwenye mchaichai una wapenzi wengi halafu ambao uko packed haujaenea sana sokoni.

Kuna Siku niliutafuta sana kwenye supermarket karibu zote sehemu ninayoishi sikuupata.

Jaribu kupack huu utamake sana mtu wangu.
 
Back
Top Bottom