Vivuko vya Azam pale feri Dar es salaam kuna dalili za Ufisadi

Kuna Watanzania hawajali kabisa pale nchi yao inapofisadiwa. Wao kwa kuwa wanapata manufaa mawili matatu baasi, hawana mpango na manufaa mapana ya Taifa.
Hawana tofauti na Wale watu wanaowashangilia majambazi kea kupora pesa kisha wakamwaga chache barabarani watu wazigombanie ili wao wasepe kiulaini!
 
Nawaza tu hapa kwa nini wasiweke hata route nyingine ya hizo sea taxi ili watu wanufaike zaidi?
 
Nawaza tu hapa kwa nini wasiweke hata route nyingine ya hizo sea taxi ili watu wanufaike zaidi?
Umesema kitu cha maana sana..waanzishe route za kuja mbezi nk..itasaidia wengi kupunguza garama za mafuta ya magari na kuleta unafuu wakati huu mgumu
 
Mbona mie naona wako sawa tu. Vinapishana vizuri tu, halafu vya Azam havipakii magari...
Kuna watu hawana shukurani na watalalamika kwa lolote lile. Ndiyo hawa wanaolalamika kuhusu Azam.

Siamini kuwa vivuko vinawekwa kwa makusudi kwa muda mrefu ili kupisha vya Azam vifanye kazi. Shaurini aondoke halafu muje kulalamika tena kuwa vivuko ni vibovu.
 
Umesema kitu cha maana sana..waanzishe route za kuja mbezi nk..itasaidia wengi kupunguza garama za mafuta ya magari na kuleta unafuu wakati huu mgumu
Hata ununio, sea breeze au mbweni pale sio mbaya
 
Kabisa, watu wanahonga sana pale ili aweze kupata nafasi ya kuvusha gari, kusubiri kwenye foleni zaidi ya masaa 8 ni kitu cha kawaida sana kama una Kigari chako.
Mumewekewa daraja bado munalalamika kukaa foleni na gari kwa muda wa masaa 8, kwa lipi?

Hayo masaa ungeshavuka kwenye daraja kwa kulipia 2000 ukaendelea na safari zako kwa buheri na afya. Watz mumerogwa na nani?
 
Hongera sana kaka, umefanya kazi ya TISS, wenye kazi yao wamelala.
 
Its like watu mnaoishi dar MNA shida sana sema mnajifanya mko sawa. Malalamiko hayaishi kila Siku ni mayowe,miano na makelele.
Hameni hamtachekwa.....kutwa kucha mnafarijiana tu kama wajawazito....maisha yenu yamejaa manung'uniko. Yaani vichwa vyenu vimejaa nywele badala ya akili.

Mnavojiona watu wa dili sasa hadi huruma.....kumbe kila MTU anamvizia mwenzake amtapeli.
 

Mumewekewa daraja bado munalalamika kukaa foleni na gari kwa muda wa masaa 8, kwa lipi?

Hayo masaa ungeshavuka kwenye daraja kwa kulipia 2000 ukaendelea na safari zako kwa buheri na afya. Watz mumerogwa na nani?
Daraja halijakamilika, bado lipo kwenye ujenzi na hayo malipo uliyasikia wapi au unatumia hisia zako tu kuleta maneno ya jeuri wakati watu wanateseka .Maamae kabisa
 
Mv magogoni na vyezake haviko salama mtakuja zama mkakumbuka mwaka 1985 baada ya kivuko kuzama na kuua woooote
Haviko salama, ila hivyo viboti ndiyo salama?
Hizo taasisi zinazosimamia usala wa vyombo hivyo hawajui kazi yao, ila wewe ndiye unayejua usalama wa vyombo hivyo?
Basi nenda kaviondoe kabisa, ili kuokoa maisha ya watu kama wewe unajua havina usalama.
 
Hujaelewa nini? Amesema kuwa kuna hujuma ya kufifisha vivuko vya umma na kuachia Azam achume kilaini. Hili jambo linaweza kuwa na ukweli ndani yake kwani hii serikali ya sasa kila mtu anashindana kupiga deal.
Nimejibu vizuri kabisa, wewe ndie hujaelewa kwasababu sioni pointi yenu ya msingi hapa, mmejawa na hisia tu zisizo na uthibitisho..

Mkisema kuna hujuma ya kufifisha, hiyo hujuma imeanza lini? kwani hivyo vyombo vya serikali havifanyi kazi sasa hivi, kama vinafanya hiyo hujuma yenu inatoka wapi? na kama vinafanya kwa kusua sua kwanini isiwe kwa sababu ya uchakavu wa miaka yote, iwe hujuma mnayoilazimisha nyie?

Mmetawaliwa na mawazo ya kupigwa ndio maana sasa kwenu kila kitu mnakichukulia kwa hofu tu, wote mnaomuunga mkono mleta mada hamna uthibitisho wa uhakika wa madai yenu, zaidi ya kuhukumu kwa hisia tu.
 

Kama vyombo vya serikali vipo na vinafanya kazi, hivi vya Azam vya kazi gani wakati siku hizi vivuko vyetu vinatumiwa below capacity?
 
Daraja halijakamilika, bado lipo kwenye ujenzi na hayo malipo uliyasikia wapi au unatumia hisia zako tu kuleta maneno ya jeuri wakati watu wanateseka .Maamae kabisa
daraja la kurasini la Nyerere halijakamilika ujenzi wake, umelala usingizi wa aina gani?

Unadhani matusi ndiyo sifa? Mjinga mkubwa wee
 
daraja la kurasini la Nyerere halijakamilika ujenzi wake, umelala usingizi wa aina gani?

Unadhani matusi ndiyo sifa? Mjinga mkubwa wee
Nahangaika na mbeba boga Fala wa kukurupuka, mi naongelea kivuko cha busisi Kigongo Mwanza na pale daraja linalojengwa ni Daraja la Magufuli liko Mwanza. wewe uko kurasini,ndo nikasema kuna uhuni wa uliopindukia kuliko hata hapo Kigamboni, watu wanahangaika kuhonga mgambo wa Suma JKT wanaolinda pale ili wavushe magari, siku ukipita hiyo njia ndo utaelewa ninachokiandika, usome comment kwa utulivu na kuelewa sio kukurupuka na mimavi yako huko
 
Mikutano ya hadhara inaenda kufumua kila uchafu na kila aliyehusika
 
Kweli kabisa Mkuu
Vivuko vya serikali vimekuwa mzigo..haviondoki kwa wakati hadi inalazimu abiria waliokuwa wamepanda kuanza kushuka kwenda kwenye kile kidogo Cha Azam.

Yaani Cha Azam kipo ng'ambo ya pili,Cha serikali kipo tu linasubiri abiria,
Cha Azam kinafika,Cha serikali hakijaondoka tu,
Cha Azam kinapakia,Cha serikali kipo tu hakijaondoka,
Cha Azam kinaondoka,Cha serikali bado kipo kimetia nanga.
Kwanini watu tusishuke?


Imefika kipindi kugombania kile Cha Azam imekuwa kawaida na ni risk maana watu wanadondoka.

Muda mwingine kunageuka bila abiria ili tu kuwahi upande mwingine,hivyo huwalazimu walinzi wafungue mlango watu wakakae pembezoni mwa maji kusubiri kuingia mara tu kikimaliza kushusha..kwa kweli kimepewa nguvu sana hivi vivuko kiasi kwamba wanafanya wanachojisikia.

All in all ,wanaoteseka ni watu wenye magari.


Hii nchi upumbavu ni mwingi sana.
 
Mv magogoni na vyezake haviko salama mtakuja zama mkakumbuka mwaka 1985 baada ya kivuko kuzama na kuua woooote
Kwamba hicho kidogo chenyewe kina guarantee ya kutokuzama?



Ambacho mara kadhaa kinanasa katikati ya maji kwa abiria kujazana mbele

Boti Kampuni moja ya Azam ikishapita na kutibua maji,basi mawimbi yake ya yanakiyumbisha sana na hakiwi stable wakati wa kutia nanga.


Ajali ni ajali.
 
Sasa wasiwasi wako uko wapi mkuu? Maana umeeleza vilevile alivyoeleza mtoa hoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…