Vivuli vya mtafutaji. (shadows of a hustler)

Joined
Jun 8, 2016
Posts
83
Reaction score
652
Jiji la dar-es-salaam limejaa vivuli vya kutafuta kwangu na vya watu wengi sana. Kila mtaa ninaopita naviona, najiona mwenyewe nilivyokua natembea hii mitaa, Kugonga milango kwenye ofisi za wahindi na kuwaelezea nini nachoweza fanya, kugonga milango hiyohiyo tena na kuambiwa nirudi wiki ijayo ili kupata malipo, wakati sijui hata jioni hiyo nitakula vipi, kugonga milango na kukutana na middle men ambao wanataka hela kidogo kabla hawajakuonganisha kwa bosi, au percent ya proposal kama ikipita.

Vivuli vya zaidi ya miaka kumi ya kutafuta na kuto kubali kushindwa, vivuli vya huu mji aisee.

Vivuli vya marafiki tuliyoenda njia tofauti, vivuli vya watu uliyodhani ni marafiki, vivuli vya december na njaanuary ambapo jua linapiga hadi kero, lakini bado tunatembea na kutafuta, maana hamna njia nyingine ukiwa mtafutaji.

Hapo kati vikaja vivuli vyenye kutia moyo kidogo, kivuli cha mara ya kwanza kushika milioni moja shilingi, aisee niliona hamna kitu kinashindikana. Nikakodi chumba cha pili kuweza expand mishe, nkasema kama milioni nmeiweza kwanini nishindwe kumi.

Kivuli cha mara ya kwanza kushika mkononi Dolari 1500 za kimarekani, maeneo ya mlimani city, nkaziweka chini ya godoro kwenye chumba changu cha elfu hamsini pale. Kijitonyama. kama mtu anakwambia hela haileti furaha anakudanganya, hela inapunguza stress, stress zikipungua furaha unaipata kupitia vingine. Hamna mwezi ambao nilipumua kama huu, ila kwa ajili kina sisi hatujawahi shika hela mda mrefu, kwa kweli sikumbuki iliishajeishaje hii hela, ila nilijifunza mengi sana. Hela haikai hata siku moja hata iwe nyingi kiasi gani, hata uweke benki gani kutunza, hela unaizungisha ikuletee hela zingine.

Ukisema ngoja nifanye a b na c kabla hujawekeza hela, utakuja jutia. Wekeza kwanza kisha inayobaki ndiyo tumia, I wish ningekua na huu ufahamu toka mwanzo.

Ila siku inafika hivi vitu vyote vinabaki kua vivuli tu.

Kama bado upo kwenye hali ngumu una tafuta ila Mambo hayaeleweki, nataka ujue kwamba inawezekana, inawezekana bila cheti hata kimoja, mimi nimeishia form 4 na nmeanza tafuta maisha tangu na miaka 16. Inawezekana, kuishi maisha ambayo unayaota kila siku, maisha bila stress ya hela. Inawezekana hii hali yako ya sahivi ibaki kua kivuli tu, Inawezekana. Inawezekana isiwe kesho au mwezi ujao, au hata mwaka ujao, ila weka kichwani kwamba inawezekana na tafuta njia nyingine.

Dunia ya sahivi imebadilika kinoma, kuna njia milioni moja na zaidi za kuingiza kipato. Ukijaribu moja na haijaleta mafao achana nayo jaribu nyingine, sikiliza "gut feeling" wenzetu wanaiita, jifunze mapya, tafuta connections zaidi.

Hakuna kitabu, hakuna mtu ambaye atakufundisha jinsi ya kufika unapotaka, wewe mwenyewe ndio njia utaitengeneza, angalia hizi semina za watu wanaofundisha mafanikio, anaefanikiwa ni nani kama siyo huyo anaefundisha. Hii ndo sababu pekee hutokuja niona nasema kwamba nafundisha mafanikio, hamna njia moja.

Mimi bado sijafika nnapotaka, msije mkadhani "ohh mkwanzania ameshatoka". Ila nina mda kidogo sijawaza hela ya chakula, hela ya kodi, naweza enda nnapotaka nikiamua, naweza wekeza kwenye ninachotaka. ila dah hili jiji lina vivuli vyangu vingi sana kila nikiwepo, naviona kila kona.

Kama umepitia mengi na sahivi hali imebadilika naomba tutaje vivuli unavyoviona ukipita sehemu, ili tuhamasishe watu wasife moyo, tuhamasishane tujenge jamii ya watu wanaosaidiana kufika malengo, maana kwa kweli tukiwa wachache kuna sehemu tutakwama, kipekee au kufika mwenyewe tu hatutofika mbali. Tupandishane wote, siku ije tuona watanzania wengi zaidi weusi waliotoka sifuri hadi kufika wanapotaka.
 
Mkuu , kwa sasa nimeondoka dar es salaam kwa ajili ya kibarua

Ila nimesha suffer sana hapo

Nilizunguka na bahasha na kuzunguka kila sehem bila mafanikio

Kila ninapopita naambiwa nitapigiwa smu ila hamna kitu aiseeee !!

Nilisuffer ila mungu hua mara zote hamtupi mja wake na daima mwenye kutafta hawezi kosa kitu

Na mm pia sjafikia pale ambapo i want to be ila sina stress juu ya nn nitakula leo au kesho au kesho kutwa ,

Sina stress ya kodi , wala balance

Namshkuru mungu kwa hapa nilipo na kupigania ninapotaka kuwepo .....

Kwenye hilo jiji lenye kila aina ya vituko aisee kivuli changu mkuu kila sehem utakikuta.
 

pamoja mkuu.. Mdogo mdogo, one step at a time tunaelekea.
 
Daah... kivuli changu bado kinanikimbiza aseeh..
 
Duh aisee me bado nasafa ila siendi lesi sana kusema kwamba nimezunguka sana ila nachokumbuka Kuna kipindi nilifikisha jembe lamilioni 1 Laki 3 ila kwabahati mbaya nikampa mimba mwanafunzi aisee jembe liliporomoka maana hata kijiwe kiligeuka kaa lamoto.

Nilichojifunza, kwenye utafutaji tujitahidi kuviepuka vitu au mazingira ambayo yatatusababishia kurudi nyuma. Kama unakahela kakodi jitahidi upange sehemu/nyumba nzuriiii isiyokuwa navibaka, jiepushe namagenge ambayo yatasababisha nawewe uonekane miongoni mwagenge hilo baya hata kama wewe ni mzuriiii maana ikitokea wakifanya tukio basi nawewe utausishwa2 so utajiingiza kwenye matatizo yatayopelekea utafutaji wako au akiba yako au mtaji wako kupotea, usijihusishe kimapenzi nawanafunzi maana ikitokea kwabahati mbaya amenasa mimba utajutia nilazima upoteze2 ili ubaki huru, chagua wanawake wakutoka nao kimapenzi maana sio kila mwanamke nimwanamke wengine nimajini kuanzia familia yake mpaka yeye mwenyewe watakufirisi.

NB: unapoanzia zero jitahidi kubagua wanawake, naikibidi kuwa na mwanamke ambaye katokea familia inayojiweza japo kwamahitaji yakawaida ili iwe nafuu kwako kukuza mtaji maana sio rahisi kutoboa huku unategemewa kwakila kitu.
 
"Sio rahisi kutoboa huku unategemewa kwa kila kitu" na kusupport kwa 100% hapo ndo utajua ni heri kuwa maskini kwenye familia tajiri kuliko kuwa tajiri kwenye familia masikini..
 
"Sio rahisi kutoboa huku unategemewa kwa kila kitu" na kusupport kwa 100% hapo ndo utajua ni heri kuwa maskini kwenye familia tajiri kuliko kuwa tajiri kwenye familia masikini..
Kabisa mkuu
 
Kivuli cha utafutaji.
Mtu anayekuonyesha picha ya gari la kifahari na ghorofa na kukumbia biashara ama mafanikio ni rahisi anakudanganya.
Kivuli cha utafutaji ni
machozi. Machozi ya kushindwa kulipa kodi na mwenye nyumba kila siku asubuhi anaamkia kwako
Kivuli cha machozi ya kukimbiwa na mke kwa kushindwa kuhudumia familia
Kivuli cha machozi cha kudharauliwa na marafiki kukukimbia
Hicho ni kivuli cha machozi cha kufilisika
Kivuli cha kukosa usingizi usiku
Kivuli cha jasho kutafuta hata kibarua cha kulipwa ef mbili ili upate chakula cha siku hiyo
Kivuli cha damu ambacho unakuwa huna hata mia mfukoni. Mwenye nyumba kafunga chumba na vitu vyako kavifungia. Simu haina salio. Simu ikipigwa ni madeni unadaiwa.
Hicho ni kivuli tu ndugu. Kubali hali halisi. Ikubali na jikubali kuwa upo chini.
Kivuli cha turn round ya kwanza kimekuja cha biashara ya ova 200mill.
The rest is history for now nna revenue ya zaidi ya 100mill a month nimeajili vijana 8.
Kivuli ninachopambana nacho kwa sasa in my late twenties ni kuhamisha biashara yangu kwa kizazi kinachofuata ama watoto wangu.
Kumbukumbu ya uchungu ulinipa discpline na for now nakaa in my own home.
Nimeeleza in short mambo niliyopitia nimetoka mkoani kuja katika kivuli cha utafutaji.
Never ever ever ever ever ever give up
 
Hongera sana kwa step ulizopiga. Haya maisha haya, ukiwa unapitia hizi hali za chini unaona kama mda hauendi, wengi sana wanakufa moyo na kurudi nyuma, wachache wanachukua opportunity na kutumia kujenga discipline, generational wealth ni muhimu sana, vizazi vinavyofuata waweze tatua mambo mengine, na kufanya makubwa zaidi. Imenigusa sana hii..
 
"Sio rahisi kutoboa huku unategemewa kwa kila kitu" na kusupport kwa 100% hapo ndo utajua ni heri kuwa maskini kwenye familia tajiri kuliko kuwa tajiri kwenye familia masikini..

At the same time ni muhimu kukumbuka kwamba hii ni majority ya watu,tunategemewa kwa mambo mengi sana, tupo connected na watu wenye hali duni, "sio rahisi sana kutoboa" in general, ni ngumu sana, mifumo ya dunia imewekwa ili tusitoke kirahisi. But inawezekana, njia zipo, ndio point ya huu uzi.
 
Good sanaa
 
Dah!! Kama vivuli vinafanana hivi....!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…