DOKEZO Viwanda vya mchina Mikoa ya Njombe na Iringa wanakata sana miti, na sisi tunafaidika kidogo sana

DOKEZO Viwanda vya mchina Mikoa ya Njombe na Iringa wanakata sana miti, na sisi tunafaidika kidogo sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Hivi viwanda vipo Iringa na Njombe. Wanakata milingoti sana na wanaharibu mazingira. Wafanyakazi hatuna mikataba anakufukuza muda wowote kwa chochote.

Assume wazee wetu walipanda miti ili watoto tufaidike, anafaidika mchina.

Kwa siku kiwanda kimoja wanaweza kata miti zaidi ya 400 na viwanda vipo zaidi ya 4.

Tunasikia kuwa walifukuzwa congo kisa kumaliza miti.
 
Miti hadi 400 ni mingi sana, haiwezekani ikatwe bila mamlaka za serikali kujua.
Suala la mikataba ya ajira hiyo naweza kukubaliana nawe.
 
Hapa mkuu tushike lipi. Ukataji miti au mikataba yenu ya ajira. Nadhani lengo lako ilikuwa kuongelea ajira na madhira yake ila kujazia nyama ukaweka na la miti.

Nikikujibu la miti, kwanza futa falsafa kwamba wazee wenu walipanda miti ili nyinyi mnufaike, walipanda kwa ajili yao na nchi yao. Nyinyi jitafutieni vya kwenu. Ninahisi serekali inajua kila kitu kuhusu ukataji huo wa miti na kama hawajui nenda karipoti haraka iwezekanavyo
 
Hivi kuna race adui wa miti kama mtu mweusi, japo sio wote!! Wanakata miti halafu hawapandi kama mbadala, nenda kwenye mapori kaone mpaka wanyama na ndege wamekimbia makazi yao kwa uharibifu wa binadamu, chunguza kwa mchina kama hawapandi mingine.....
 
Wachina wachapa kazi sana
Waswahili uvivu na wizi wachina watawafukuza sana Kazini

Nawaunga mkono waendelee kuwatimua tu Hadi akili zenu zike sawa
 
Haiwezekani miti/misiti inajaliwa pamoja na tembo kuliko mtanzania. Bora ikatwe tu na hao Tembo kuuliwa.
 
Wanakata miti kwenye shamba la nani ?

Je wanavamia mashamba ya watu na kukata miti ya watu ambayo hawajaipanda wao ?
 
Back
Top Bottom