A
Anonymous
Guest
Mimi ni mkazi wa Kinondoni shamba, kata ya Kinondoni. Mwishoni mwa wiki iliyopita 23.11.2024 nilikunywa maji ya Dawasco ila kitu cha kushangaza yalikuwa na harufu kali sana ya dawa na pia kulikuwa na ladha ya uchungu kwa mbali.
Kwa kuwa ilikuwa weekend nilipumzika kidogo muda wa mchana. Nilipoamka nilishangaa kuona malengelenge (vipele vilivyojaa maji) kwenye kwenye ngozi mkono wa kulia na kushoto. Nikajua labda ni vipele vya joto lakini kadri nilivyoendelea kunywa yale maji, vipele vinaongezeka.
Usiku wa Jumapili jioni nikaamua kununua maji dukani ili nione kama kutakuwa na mabadiliko, leo Jumatatu nimeamka vipele vimekauka.