Niaje wadau. Kuna kampuni imekuja kutangaza kuwa inauza viwanja Mlandizi. Ikatoa na ramani na inasema unaweza kulipa kidogokidogo ndani ya miezi 18 unatakiwa uwe umemaliza.
Sijawahi kufika huko Mlandizi Ila kampuni ina ofisi na hata namba za akaunti na simu walizotoa zimesajiliwa kwa majina ya kampuni. Nilifika hadi ofisini kwao. Ukigawa Bei ya kiwanja kwa hiyo miezi 8 unatakiwa kulipa 90,000 kila mwezi.
Ila unaweza kulipa zaidi au kidogo Ila unatakiwa ndani ya miezi 18 uwe umemaliza. Najishauri nijiingize kulipa kidogokidogo au niache. Naombeni ushauri wenu.