Viwanja vya Mwadui, Manungu na Mabatini vyafungiwa kutumika msimu huu

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Bodi ya Ligi limevifungia viwanja vitatu uwanja wa Mwadui, Manungu na Mabatini kutumika katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara hadi hapo vitakapofanyiwa marekebisho.

Akizungumza Dar es Salaam, Afisa mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura alisema viwanja vilivyofungiwa ni pamoja na uwanja wa Mwadui, Manungu na Mabatini.

Alisema sababu za kufungia viwanja hivyo ni kubainika uzio wake unamapungufu ni hatari kwa wanasoka wenyewe kwa mfano uwanja wa Manungu, Mabatini vyote vimezungushiwa mabati wakati Mwadui imezungushiwa makuti.

"Ukaguzi wa viwanja unaendelea na tayari tumesha fungia viwanja vitatu kwa sababu zilizotajwa na tumeshawatengea viwanja watakavyotumia msimu ujao na kuwa viwanja vyao vya nyumbani," alisema na kuongeza kuwa.

"Mtibwa watatumia uwanja wa Jamhuri, Ruvu Shooting watatumia Isamuyo na Mwadui watatumia Kambarage watarudi kwenye viwanja vyao hadi hapo watakapomaliza ukarabati," alisema Wambura.
 
Hatati sana, quality management kwetu huwa ni msamiati
 
Mtibwa hapo wamefurai, maana wanapenda kuchezea jamhuri ila wanakosaga nafasi, sababu ya mashabiki kuwa wengi kuliko kule mbali manungu
 
Write your reply...Safi sana TFF, Ila mmeangalia uzio peke yake VP kuhusu pitch
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…