Viwanja vya Uwanja wa Taifa, Azam Compex na viwanja vya Maonyesho vya Sabasaba huenda vikafungwa

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imetangaza dhamira ya kuvifungia viwanja vya Uwanja wa Taifa, Azam Compex na viwanja vya Maonyesho vya Sabasaba kwa kuwa wamiliki wa viwanja hivyo hawajawahi kulipa kodi ya ushuru wa huduma tangu vijengwe.

Akizungumza Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Lusubilo Mwakibibi amesema kuanzia jana wamiliki wa viwanja vya Uwanja wa Taifa na Azam Compex watafute viwanja vingine vya kuchezesha mechi ambazo wanazo kuanzia sasa kama hawatalipa kodi hiyo.

Mwakibibi alisema kodi ya ushuru wa huduma hiyo wanayohitaji halmashauri ya manispaa hiyo ni asilimia 0.3 ya mapato wanayoingiza kila uwanja unapotumika .

"Hatuwezi kuendelea na utaratibu huu mfano sasa hivi kuna maandalizi ya sabasaba katika viwanja vya maonyesho vya Sabasaba pamoja na viwanja vya uwanja wa Taifa na Azam Compex kuna mechi zinaendelea ninawatuma watu wetu waje kuzuia kwenye milango kisifanyike kitu chochote hadi hapo mtakapolipa kodi ya ushuru wa huduma,"alisema Mwakibibi.

Alisema akishawaandikia barua tangu mwaka 2018 wawe wameshalipa kodi hiyo ifikapo Aprili Mosi lakini hakuna hata mmiliki wa viwanja hivyo aliyeenda kulipa kodi hiyo.

Mwakibibi alitolea mfano wa Uwanja wa Taifa walipowakumbusha wamekuwa wakipiga danadana mara wanaohusika ni Serikali Kuu mara ni Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) .Pia upande wa Azam Complex walionyesha nia ya kulipa lakini wamekuwa wakiwazungusha bila mafanikio.

Na upande wa viwanja vya Maonyesho vya Sabasaba wao walionyesha nia ya kufanya mazungumzo lakini baadaye waliieleza halmashauri hiyo anayetakiwa kuzungumza hayupo.

Alisema kinachohitajika wamiliki wa viwanja hivyo walipe kodi wakumbuke hivi karibuni ilichezwa timu ya taifa ya Uganda na Tanzania watu walijaa hadi nje ya uwanja watu walitupa ovyo uchafu kazi ya halmashauri ni kusafisha lakini hawakupewa fedha ya kodi ya ushuru wa huduma.

Mwakibibi alisema wanapokusanya kodi hiyo inasaidia kuwalipa watu wanaofanya usafi pembezoni mwa barabara za halmashauri hiyo na pia wana uhaba wa vyumba vya madarasa hivyo fedha hizo zitasaidia kujenga madarasa 140.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HHuyo Mnyakyusa tutampima kwa makusanyo anayoingizia halmashauri ya Temeke, maana Kila Siku ana matamko mapya, soon tutasikia wenye madishi ya TV mkayalipie manispaa
 
Huyu bwana kabibi. Nadhani amekurupuka bila kufuata taratibu. Wewe unajua taratibu zote za kiserikali. Leo unakurupuka nakutoa matamko ya vitisho wakati unajua kuna michezo mikubwa wikiendi hii? Huyu ameshiba ajira yake.
 
Kuna utitiri wa kodi usio na tija. Hebu fikiria hivyo viwanja vya mpira; kodi VAT 18%, Zimamoto ...%, BMT....%, TFF .....% Chama cha soka cha Wilaya....%, Chama cha soka cha mkoa.....%, Manipaa
03% , bado kuwalipa wafanyakazi, hivi kuna kitu wamiliki wanapata kweli?

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtatuua jamamani, BMT,TRA,USHURU WA UWANJA na nyie tena mmekuja
Mie nipo Ilala wenye biashara tumeshawazoea huwa tunakutana na municipal kila baada ya miezi mitatu,ifikie mahali pande zote tuwajibike kwenye kodi mbalimbali zinazobuniwa japo sometimes huwa za ujanja ujanja.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Mwakibibi alisema kodi ya ushuru wa huduma hiyo wanayohitaji halmashauri ya manispaa hiyo ni asilimia 0.3 ya mapato wanayoingiza kila uwanja unapotumika .
nijuavyo kodi hii hulipwa kila baada ya miezi mitatu Yaani 0.3% ya mauzo yako ya miezi tatu
 
Hata kwenye biashara za kawaida aneleta usumbufu mwingi mno ! namtabiria kuhamishwa haraka sana , kuiba kura kila mkurugenzi anaweza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…