Vizazi vilivyopita

Guasa Ambonii

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2015
Posts
8,545
Reaction score
10,283
Ndugu zangu inaweza kuwa hili limeisha letwa hapa jamvini ila si vibaya kujikumbusha.

Nimejaribu kuvuta kumbukumbu ya soka kuna vizazi vitabaki penye historia nitaanza na brazil ya mwaka 70 hii iliwajumuisha garrincha,Pele,vava,didi tostao revelino na wengine hiki kikosi Italy alikula bao 4-1 watu wengi husema hakuna kikosi bora kwa brazil kama hicho.

Kingine kwa ngazi ya vilabu naanza na man united ya miaka ya 60 hapo unakutana na George Best Denis law na mtu mzima Charlton huo ulijulikana kama utatu mtakatifu na walitwaa kombe la ulaya na kuja kufuatiwa na watoto wao hii ni miaka ya kuanzia 94 hapo ujio wa Beckham,nick butt,Neville brothers,giggs na Scholes khabari zao zinajulikana.

Ukija Arsenal hiyo ya ukuta wa chuma wakongwe watupu seamen, Lee dickson,winterburn na baba mwenye nyumba Adams hapo ilikuwa kazi kweli..

Wadau tunaweza kuungana kwani kila mtu ana kizazi chake.
 
Kuna kizazi cha dhahabu cha Nigeria kilichotwaa Olimpiki 1996 na Caf 1998 kikiwa na akina Nwanko Kanu,JJ Okocha,Taribo West,Tijan Babangida,Celestine Babayaro,Finidi George,Victor Ikpeba,Jonathan Akpoborie.
 
Kuna kizazi cha dhahabu cha Nigeria kilichotwaa Olimpiki 1996 na Caf 1998 kikiwa na akina Nwanko Kanu,JJ Okocha,Taribo West,Tijan Babangida,Celestine Babayaro,Finidi George,Victor Ikpeba,Jonathan Akpoborie.
Hicho nakumbuka Spain anakula 3 moja kati ya bao zuri lilikuwa la Sunday oliseh nje ya kumi na nane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…