SoC01 Viziwi na walemavu wengine wamesahauliwa na Serikali juu ya vita dhidi ya Corona?!

SoC01 Viziwi na walemavu wengine wamesahauliwa na Serikali juu ya vita dhidi ya Corona?!

Stories of Change - 2021 Competition

Emmanuel Nelson

New Member
Joined
Jul 22, 2021
Posts
2
Reaction score
1
Covid - 19 ni ugonjwa unaosabishwa na virusi vya corona. Ugonjwa huu kwa ambao upo kwa takribani miaka miwili sasa unasambazwa kwa njia ya hewa toka kwa mtu mmoja aliye athirika kwenda kwa mwingie. Lakini pia ugonjwa huu umekuwa ukisambaa kwa kasi na kusababisha vifo vya mamilioni ya watu duniani kote mpaka sasa

Kutokana na kasi ya uenezwaji wake na idadi ya vifo kuzidi kuwa kubwa, ugonjwa huu sasa umekuwa ni janga la dunia na hivyo kupelekea serikali nyingi duniani kuchukua tahadhari kadha wa kadha katika kujaribu kuudhibiti ugonjwa huu.

Serikali yetu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ni moja wapo ya serikali zilizoanza kufanya jitihada katika kudhibiti ueneaji wa ugonjwa huu hatari wa Covid - 19 kwa kuwataka raia wake wachukue tahadhari kwa kuepuka mikusanyiko isiyokuwa ya lazima, kuvaa barakoa au kunawa mikono kwa maji tiririka mara kwa mara.

Lakini pia Serikali imetangaza kuanzia leo itaanza kugawa chanjo bure kwa makundi maalum ambao ni wahudumu wa afya na watu wenye umri mkubwa! kinacho nishangaza hapa ni kwamba katika matamko yake yote serikali yetu tangu hili janga liingie hatujaona wakitoa waraka maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu wanasaidikaje na janga hili

Mfano watu wenye ulemavu wa kusikia, hapa tumeshuhudia viongozi wa kitaifa wakija na matamko kadha wa kadha lakini hatukuwahi kushuhudia hata mara moja kwenye matamko yao wakiambatana na wakalimani wa lugha za za 'ALAMA' kwa ajili ya ndugu zetu wenye ulemavu wa kusikia (viziwi) nao wapate ujumbe husika uliokusudiwa kuwasilishwa

Pia hata kwenye vipeperushi na maandiko kadhaa rasmi yanayotolewa na serikali yetu hatujaona pia yale ya 'NUKTA NUNDU' kwa ajili ya ndugu zetu wenye ulemavu wa kuona(vipofu) ili na wao pia wapate ujumbe sawasawa na wanaoupata watu wasio na ulemavu!

Hivyo basi kwa kuhitimisha ningeishauri Serikali, inaposema itaanza kugawa chanjo kwa makudi maalum ingewajumuisha pia watu wenye ulemavu mbalimbali kama viziwi, vipofu, viwete n.k ili nao waweze kuwa salama dhidi ya janga hili la Corona. Hili linawezekana kwa kuweka vituo maalum kwa ajili yao tu kwenye maeneo tofauti tofauti nchini hasa kwenye shule zao za watu wenye mahitaji maalum kwani shule hizi tayari tunazo kwenye maeneo mengi ya nchi yetu.

Pia inapoonda huko iende na wakalimani wa lugha za alama na maandiko ya nukta nundu ili ujumbe ufike kwa usahihi na urahisi zaidi. Kwa kufanya hivyo Serikali itakuwa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupambana na janga hili la Covid - 19 kwa watanzania wote pasipo kujali tofauti zetu za maumbile ambazo wengi ni za kuzaliwa nazo na sio kusubiri kila jambo mpaka tupewe miogozo na mashirika na taasisi za kimataifa bali tuwe wabunifu sisi wenyewe na wengine waige toka kwetu.

Ashante.
Emmanuel Nelson.
+255714 828 834
mpelangwa@gmail.com
 
Upvote 1
Back
Top Bottom