Voda kazi inawashinda, kama tatizo ni miradi mingi punguzeni.

Voda kazi inawashinda, kama tatizo ni miradi mingi punguzeni.

Mzee wa ngano

Senior Member
Joined
May 3, 2012
Posts
184
Reaction score
54
Katika maswala ya biashara siku zote mtu anatafuta jina kwanza ndipo huweza kufanya biashara yake kwa uhakika. Ili mtu apate jina kwa biashara yake kuna mambo mengi tofauti tofauti ambayo kwayo mtu akiyafanya hupata kujulikana na biashara yake huwa nyepesi.
Hawa jamaa zangu wa voda wamepata jina na wamefanya kazi kubwa pengine kupita mitandao mingine yote hapa nchini lakini sasa hivi naona wamekuwa wabovu kuliko mitandao mingine yote.
Utakuta mtu eti unampigia simu akipokea au hata kabla hajapokea unajisikia mwenyewe,
au unanunua umeme wa LUKU kwa M-Pesa then hupati huo umeme for long,
au unamtumia mtu pesa kwa M-Pesa zinaingia kimya kimya au haziji kabisa wakati kule kwa sender zimeshakatwa.
Haya na mengine yamekuwa ni matatizo ya kudumu kwa sasa hasa ukiwa mkazi wa Tabora.
Wanangu wa voda kama mpo hewani badilikeni mtaharibu kazi.
 
sio tabora tu,hata huku dar mambo ni hayo hayo tu,karibia wiki sasa,kwakeli wanachosha
 
Huku njombe voda ndio matatizo usisema, unampigia mtu hapatikani lakini simu iko hewani, au akipokea tu inakatikatika ghafla, ukiwapigia custom wanakwambia piga maranyingi zaidi ndio itakubali, sasa kama umevamiwa na majambazi si ndio umekwisha.
 
hiyo ya kupiga halafu ukajisikia nilidhani simu yangu mbovu..dah!...kumbe
 
Ni kheri kuwa na wateja wachache na ukawahudumia kwa ubora stahiki kuliko kuwa na wateja lundo na kila kitu ni bora liende na ndicho wafanyacho voda base kubwa ya wateja na utitiri wa huduma vyawapa kichwa bila kusahahu daily most of their customers are getting pierced off
 
Huku njombe voda ndio matatizo usisema, unampigia mtu hapatikani lakini simu iko hewani, au akipokea tu inakatikatika ghafla, ukiwapigia custom wanakwambia piga maranyingi zaidi ndio itakubali, sasa kama umevamiwa na majambazi si ndio umekwisha.

hapo kwenye red, sidhani kama wako serious na biashara yao,hilo ni jibu la kitoto sana.Mimi mwenyewe nimeishagombana na wife mara nyingi kweli kuhusu hiyo voda,unapiga unaambiwa namba haiko hewani,lakini yeye anakuambia sijazima simu mda wote nilikuwa hewani.Kweli hawa jamaa warekebishe,wanatutafutia ugomvi bure na kukosa taarifa za muhimu.
 
Back
Top Bottom