Mzee wa ngano
Senior Member
- May 3, 2012
- 184
- 54
Katika maswala ya biashara siku zote mtu anatafuta jina kwanza ndipo huweza kufanya biashara yake kwa uhakika. Ili mtu apate jina kwa biashara yake kuna mambo mengi tofauti tofauti ambayo kwayo mtu akiyafanya hupata kujulikana na biashara yake huwa nyepesi.
Hawa jamaa zangu wa voda wamepata jina na wamefanya kazi kubwa pengine kupita mitandao mingine yote hapa nchini lakini sasa hivi naona wamekuwa wabovu kuliko mitandao mingine yote.
Utakuta mtu eti unampigia simu akipokea au hata kabla hajapokea unajisikia mwenyewe,
au unanunua umeme wa LUKU kwa M-Pesa then hupati huo umeme for long,
au unamtumia mtu pesa kwa M-Pesa zinaingia kimya kimya au haziji kabisa wakati kule kwa sender zimeshakatwa.
Haya na mengine yamekuwa ni matatizo ya kudumu kwa sasa hasa ukiwa mkazi wa Tabora.
Wanangu wa voda kama mpo hewani badilikeni mtaharibu kazi.