Fohadi
JF-Expert Member
- Jul 24, 2020
- 772
- 2,421
Hii ni kama mara ya tatu inanitokea. Mara ya kwanza nilihisi labda nimekosea. Nikasema basi bahati mbaya nimekosea. Yapili tena nikashituka nikasema hapa nimepigwa. Hii ya tatu sasa nimeamini wanachofanya hawa jamaa ni utapeli kama utapeli mwingine.
Iko hivi,
Kabla sijajiunga na kifurushi huwa naangalia menu iliyopo mezani ili kuchagua ni kipi kitanifaa kutokana na mahitaji husika. Asilimia 90% ya vifurushi vyangu ni weekly bundles.
Siku ya kwanza, nimeangalia Menu nikakuta kuna kifurushi cha week 1500/= ambacho kitanifaa. Nilipoweka vocha sh. 1500 nikarudi kwenye menu kujiunga nikakuta kile kifurushi hakipo, na cha aina ile kipo kwa 2000. Nikahisi labda nilikosea kuangalia. Sikuona shida nikaongezea 500 nikajiunga. Siku ya pili pia ikawa hivyo hivyo ndipo nikashituka.
Sasa leo imenitokea hadi nimeamua kuandika uzi huu. Mida fulani baada ya bundle langu kukaribia kukata. Nikaamua kununua vocha. Ila kabla sijanunua, nikaangalia menu kuona kipi kitanifaa. Baada ya kuridhika na kifurushi cha 1500/= nikachukua hela nikanunua vocha. Baada ya kujaza vocha ya 1500 nikarudi kwenye menu kujiunga. Lahaula!!!, nikakuta kile kifurushi cha 1500 kimekuwa 2000. Ndani ya dakika 2 menu imebadilika.
Baada ya hapo nikaamua kuongezea tena hiyo sh. 500 ili niweze kujiunga cha 2000 kama walivyotaka. Sasa cha ajabu, nimeongeza sh. 500 ikawa 2000. Niliporudi kwenye Menu kujiunga hicho kifurushi, nikakuta tena cha 2000 hakipo. Wameweka tena 1500. Haya yote yanatokea ndani ya dakika 1. Ikabidi nijiunge hicho cha 1500 na kuiacha hiyo 500 ina hang na ninauhakika watapita nayo juu kwa juu....Wizi.
VODA badilikeni. Huu ni wizi. Na kama mnataka kuuza vocha hii sio mbinu sahihi. Haiwezekani unambie 1500, nikiweka vocha ya 1500 unanambia tena hiyo bundle 2000. Naongeza 500 inakuwa 2000. Naingia kujiunga tena mnanambia hicho kifurushi ni 1500 na cha 2000 hakipo.
Kwahiyo mlitaka kuuza vocha au nini? Mambo ya ajabu kabisa mnafanya na mnawaumiza wateja wenu. Matakle yenu!!!