Vodacom acheni hii hujuma kwa Watanzania!

Ndebile

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2011
Posts
7,745
Reaction score
11,267
Kwanini kutuma pesa kutoka Voda kwenda Voda inakuwa rahisi na huduma inakuwepo muda wote ila kutuma mtandao tofuti mnasuasua! Leo kuanzaia saa kumi na mbili asubuhi hadi sasa hivi saa nne huduma ya kutuma pesa kwenda mtandao mwingine hakuna! Tatizo hili sio leo tu bali limekuwa likijirudia mara kwa mara.

Baada ya kuona watu wengi wanatumia M-Pesa kununua vifurushi vya muda wa maongezi na data kwenye mitandao mingine ambayo bei zao za huduma zipo chini kuliko ninyi ndio mkaja na mkamkati huu.

Endeleeni na ujinga huu tuone kama hata hiyo Mpesa watu hawataikimbia!
 
Pole mkuu.

Mimi natumia Voda tangu 2012 sijawahi kuona hili tatizo.
 
Hivi kwa nini voda ukiweka salio bila kujiunga kesho hulikuti
 
Sasa hivi wamenipiga 1000 yangu, nilikuwa natoa mpesa kupelega tigo pesa ili ninunue hitaji langu,ghafula ikaja SMS "samahani muamala wako haukukamilika kwa sababu za kiufundi,tafadhali wasiliana na huduma kwa mteja"MBAYA ZAIDI wamekata pesa kutoka KWENYE salio langu LA mpesa, how come this? Inauma sana kuna SIKU hili lilitokea nikajua watanirudishia ndio ikawa kwa heri ya kuonana.
INAUMA SANA.
wamenifanyia hili SAA 11:38 about 30min ago.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…