Wizi mkubwa mitandao ya cmu za mkononi, unaweza kujiunga na kifurushi alafu baada ya mudafupi kabla hata ya kupiga cm wala sms wala internet lakin ukajikuta huna hata kimoja na salio la vocha nalo halipo! kilichotokea nikwamba wanakata salio lako na kukutumia sms ya kukudhibitishia kua umenunua kifurushi, kumbe hata hujapewa kile kifurushi! pengine haya ni makosa ya kiufundi lakin mbona hata hawarudishi pesa zetu hata pale tunapopiga cm huduma kwa mteja?
Ukifanya malipo kwa m pesa na ikatokea tatizo kwenye mtandao pesa yako ndo vile tena inapotea!
Sasa hivi mtandao kama voda umekua mzigo sana kwa wateja wake, kila cku matatizo mara cm hazipatikan japokua inaonyesha mtandao upo na wakati mwingine sms ya jana unaipokea leo nam yako ipo hewab masaa 24.
KIKUBWA ZAIDI
Serikali imetoa agizo kua gharama za kupiga cm nje ya mtandao ni Tzs.34 kiwango cha juu kabisa! leo kinachoendelea nitofauti kabisa, eti ili uupige cm kwa bei ya 34 kwa dakika inabidi unubue kifurushi cha 350 tsh. Upate dakika 10 kwa maana nyingine lile agizo kwetu imekua kama msaada ambao masharti yake nikwamba lazima uwe na salio lisilopungua 350 ambalo utalitumia ndani yz masaa 24! kwakweli huu nao ni wizi, kwanini inolazimishe kutumia 350 kwa cku, kinachotakiwa ni kuweza kutumia tzs 34 kila unapopiga cm kwa dakika 1 halafu kama wameamua kutoz offa kwa wateja basi iwe chini ya 34 kwa kilz dakka vinginevyo watakua wanatukaanga kwa mafuta yetu wenyewe!