Vodacom: Baada ya ujio wa Tozo, mapato ya MPESA yameshuka kwa 13.9%

Imagine transaction zinazofika 6.5 trillion kwa mwezi huu mtandao mmoja tu halafu mwigulu anasema serikali imekusanya 50 billion tu kwa tozo za miamala?

Tuchukue wastani wa 1000 tu kwa kila muamala tuone jibu ni sh.ngapi?

1000*6,500,000,000,000=

Hizi tozo tunapigwa sana!
 
Shukrani zote zimwendee Mama kwa kuupiga mwingi!
 
Inawezekana . Mfano mimi nikimtumia mtu milioni 1 na yeye akaenda kuitoa hiyo Milioni 1. Hizo tayari ni transaction mbili lakini pesa ni ile ile moja. Ingawa transaction ni za milioni mbili.
 
Inawezekana . Mfano mimi nikimtumia mtu milioni 1 na yeye akaenda kuitoa hiyo Milioni 1. Hizo tayari ni transaction mbili lakini pesa ni ile ile moja. Ingawa transaction ni za milioni mbili.
Sawa ila we ukituma unakatwa hela na yeye anakatwa hela unless umpe wakala amuwekelee direct!

Still hata ukigawa miamala halfway, say 3trillion ukizidisha kwa wastani wa buku tu ni hela ndefu sana sio billion 50 tu! Huko ni voda tu, kuna tigo na airtel!
 
Safi Sana eti wanajisifu wamekusanya mabiolioni ya tozo watu wameshajua kwa sasa hawafanyi miamala serikali ya kijinga Sana hii
 
Kuna kipindi voda wametangaza kupata faida? Maana kila nikiwafuatilia wao ni hasara tu.
 
Serikali ilitaka mitandao isajiliwe soko la hisa ili kuleta uwazi... sasa uwazi unawaumbua.

Nani alisema hakuna madhara ya tozo kwa wananchi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…