haibreus
JF-Expert Member
- Oct 1, 2009
- 295
- 106
Nakaribia kuhamia airtel kwa kweli maana nina bundle za voda za kutosha lakini nakosa huduma ya internet,mpesa pia hata huduma ya voice hapa kwetu ni mbaya yani wananchi wengi wa hapa wanalalamika naomba tu nitaje na eneo lenyewe kuwa ni mabibo hostel.ukiwa mbele ya majengo ya mabibo hostel yani katika maduka yote na sehemu mbalimbali za biashara huduma iko very slow ya internet ya vodacom na voice ni mbovu sana yani ukipiga simu hamsikilizani na ina katika katika hadi usogee karibu na barabara ya lami na ukichunguza utagundua kuna mnara wa vodacom upo nyuma ya majengo ya mabibo hostel ambao umezuiwa na majengo pia kuna mwingine upo maeneo ya external na unaitwa mabibo ambao upo chini sana na ninadhani haukumaanishwa kutupatia huduma sisi wakazi wa hapa mbele ya mabibo hostel.Vodacom tunawaomba mlifanyie kazi hili kwa kuwa tumewazooeni na pia tunapata hasara kwa huduma zetu za internet cafe na biashara zetu pamoja na elimu.Mimi ninaishi karibu kabisa na mnara wa airtel hapa mbele ya majengo ya mabibo hostel kwa hiyo ili kuthibitisha nisemayo nawaombeni mfike mahali hapa na mshuhudie hasara tunayoipata kutokana na service kuwa mbaya sana hapa.
Vinginevyo ninaendelea kupata raha na airtel na kwakweli nikiizoea huduma hii basi vodacom mtakuwa mmenipoteza mimi kama mimi kwani nipo na nyie tangu 2001 na sitafurahi kuwaacha. Na ninaweza kuwapatia namba yangu mkihitaji ili muone mimi binafsi ni mteja wa aina gani kwenu .Nina imani kuwa masikio yenu yanafanya kazi
.nawakilisha