Vodacom chondechonde

haibreus

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2009
Posts
295
Reaction score
106
Nakaribia kuhamia airtel kwa kweli maana nina bundle za voda za kutosha lakini nakosa huduma ya internet,mpesa pia hata huduma ya voice hapa kwetu ni mbaya yani wananchi wengi wa hapa wanalalamika naomba tu nitaje na eneo lenyewe kuwa ni mabibo hostel.ukiwa mbele ya majengo ya mabibo hostel yani katika maduka yote na sehemu mbalimbali za biashara huduma iko very slow ya internet ya vodacom na voice ni mbovu sana yani ukipiga simu hamsikilizani na ina katika katika hadi usogee karibu na barabara ya lami na ukichunguza utagundua kuna mnara wa vodacom upo nyuma ya majengo ya mabibo hostel ambao umezuiwa na majengo pia kuna mwingine upo maeneo ya external na unaitwa mabibo ambao upo chini sana na ninadhani haukumaanishwa kutupatia huduma sisi wakazi wa hapa mbele ya mabibo hostel.Vodacom tunawaomba mlifanyie kazi hili kwa kuwa tumewazooeni na pia tunapata hasara kwa huduma zetu za internet cafe na biashara zetu pamoja na elimu.Mimi ninaishi karibu kabisa na mnara wa airtel hapa mbele ya majengo ya mabibo hostel kwa hiyo ili kuthibitisha nisemayo nawaombeni mfike mahali hapa na mshuhudie hasara tunayoipata kutokana na service kuwa mbaya sana hapa.
Vinginevyo ninaendelea kupata raha na airtel na kwakweli nikiizoea huduma hii basi vodacom mtakuwa mmenipoteza mimi kama mimi kwani nipo na nyie tangu 2001 na sitafurahi kuwaacha. Na ninaweza kuwapatia namba yangu mkihitaji ili muone mimi binafsi ni mteja wa aina gani kwenu .Nina imani kuwa masikio yenu yanafanya kazi
.nawakilisha
 

Bob airtel ndio kila kitu....Kwanza bundle zao mpya za kupiga mitandao yote at one cellular price ni funika so far sijawah ona !!! Hata kwa kawaida cost za kupga na sms zko cheap sana. Mitandao mingne nshatia kapuni siku nyngi. tiGO nao ovyo sana !!
 
Ni kweli kuwa voda huwa wanasumbua sana na bando zao, hasa usiku. Mbaya zaidi hili tatizo wanalijua ila ndio hivyo tena
 
Vodacom hovyo kabisa na hata huduma yao ya mpesa hovyo kabisa sitaki hata kuisikia kwani ninapotumia hairudishi majibu kuwa muamala umefanikiwa au la ukipiga huduma kwa wateja ndo usiseme sijui wanakuwa wamelala? Nimemua kuamia mtandao mwingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…