Vodacom + HESLB

mbota

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
1,054
Reaction score
585
Vodacom mmepewa tenda na bodi ya mikopo kwa ajili ya malipo ya maombi ya mikopo ila kwa nini vodacom M PESA Haitaki kufanya hayo malipo toka asubuhi tunajaribu kulipa hapa ila majibu yenu ni kwamba reference au namba ya form four tunakosea wakata tunafuata vigezo na masharti sasa nyie vodacom ndio mna maana gani? wahudumu wa vodacom wenyewe wanashindwa kutoa jibu....
na kama kuna tatizo kwanini msitoe tangazo kwambo kuna tatizo?
sasa vodacom isumbue bado website ya bodi isumbue kweli ndio tekohama hiyo tunayohitaji watanzania au mna force mambo
:faint2::faint2::faint2::faint2:
 
Huduma, hizi, noma branch ipo mbagala unaambiwa niende mlimani siti kwa ajili ya muamala shikamoo Vodacom
 
mi nimelipia ila kila ninapoingiza transaction id wananijibu invalid. Yaani, wamenipotezea siku kabisa.ngoja nijaribu jesho
 
Haya, mambo, bana sijui, kwann, wanazingua, hivi
 
Hii nchi inakurupukaga na kujiingiza kichwakichwa tu ktk mambo ya technology
 
Hii nchi inakurupukaga na kujiingiza kichwakichwa tu ktk mambo ya technology

Yani wanakosea sana mimi nipo town je aliyepo kule interior si ndio mbaya zaidi Vodacom jirekebisheni na hao waudumu wenu wapeni semina jinsi ya kujibu maswali mhudumu anakujibu, sijui hiyo nn, na, products ni ya, Vodacom duu
 
yani wanakosea sana mimi nipo town je aliyepo kule interior si ndio mbaya zaidi vodacom jirekebisheni na hao waudumu wenu wapeni semina jinsi ya kujibu maswali mhudumu anakujibu, sijui hiyo nn, na, products ni ya, vodacom duu






na time ndiyi hii inaenda kuisha
 
Hawa Bodi ya Mikopo kama wanasoma huku tafadhali rekebisheni system yenu, inasumbua sana, na number ya simu mliyoweka haipatikani.

Aactually mmeweka number moja tuu ambayo ni +255 22 550 7910, hiyo number inapigwa na Tanzania nzima haipatikani kabisa, tukija ofisini kwenu, mlinzi anakwambia tumeambiwa tuwaambie mjaribu kupiga mara nyingi mpaka ipatikane, (kumbuka siku zinaisha maana deadline yenu ni tarehe 30)

Ukikutana na mlinzi kashiba vizuri na ana raha siku hiyo anakuruhusu uende reception, kimbembe ndio kinaanzia hapo reception sasa. Pale reception wanajibu majibu ya hovyo sana, tena hata hakuangalii usoni, wakati anakujibu anasoma gazeti na hawana msaada kabisa na watu zaidi ya wao kusoma gazeti, unauliza kitu kama mbona nimelipia lakini kila nikitaka kuingia kujaza form inakataaa? husaidiwi unajibiwa utumbo na mtu anaendelea kusoma gazeti.

Kuna kaka pale na dada wa kiarabu, ni shidaaa, afadhali huyo kaka anakujibu angalau vizuri japo hawana msaada, huyo dada wa kiarabu anajibu utumbo mmoja tuu anakuwa hana habari tena na wewe na akiona unamuuliza sana hakujibu chochote anaendelea kusoma gazeti. Hii ni mbaya sana. Watu wengi wanalalamika, maana watu wametoka mbali wanapoteza nauli zao kuja mpaka kwenu halafu mnashindwa kuwasaidia.

Eti majibu yenu ni nyie hamna uwezo wa kuwasaidia zaidi ya kuendelea kupiga simu, sasa apige vipi simu wakati simu yenyewe haipatikani na hata ikipatikana haipokelewi. Kwa kweli mnatunyanyasa sana wanafunzi!

Basi ingekuwa afadhali mchukue hayo malalamishi myapeleke kwa wausika wakati mwanafunzi anasubiri jibu, hamfanyi hivyo nyie mnajibu ndio tulivyoambiwa tuwajibu hivyo, na hamruhusiwi kuonana na wafanyakazi face to face, ni kitu gani hichi jamani?? Kama mnasoma hapa tunaomba mjirekebishe please!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…