Vodacom: hivi ni kwa nini lakini?

Vodacom: hivi ni kwa nini lakini?

TANMO

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2008
Posts
11,763
Reaction score
11,873
Siku hizi hawa Jamaa wamekuwa na mtindo wa kutujazia wateja Inbox zetu kwa Meseji juu ya Products/Services zao mpya (ambazo hata hivyo huwa hazidumu).. Hii ni Tabia ya Tigo, Voda wameamua kuiga?
Siku hizi Vodacom wamekuwa wakianzisha Products/Services ambazo huwa hazikai sana, wanaziondoa.
Siku hizi Menu ya Vodacom inabadilika badilika kila mara bila maboresho ya msingi (wakati mwingine haipatikani)
Je kitengo cha Masoko cha hii Kampuni hakifanyi Utafiti na kujiridhisha kabla ya kuruhusu bidhaa iingie sokoni?
Yaani ni kama vile wako desperate na kitu fulani hivyo wanakurupuka kufanya maamuzi ili wajiokoe..
Hii Bima ya Vodacom faraja ni kama kuwaambia watu kufeni ili tuwalipe ndugu zenu, kwa nini hawakuanzisha Bima ya Afya ili inufaishe watanzania wenye mahitaji ya huduma za Afya (na kuwaepusha na vifo) kuliko kusubiri tufe ili watoe kifuta machozi kwa ndugu zetu?
Kwa upande wa M-Pesa pia kuna matatizo ya mara kwa mara, message delay, transaction cancellation n.k

Binafsi nauchukulia huu Mtandao kama 'wenye afadhali' kulinganisha na mitandao mingine, lakini hizi kero za mara kwa mara zinakatisha tamaa sasa.

Rene Meza, hebu rekebisha hizi kero Bana.

Mapendo
TANMO
 
Back
Top Bottom