mr pipa
JF-Expert Member
- Jul 26, 2021
- 3,074
- 6,472
Tangia mwaka jana mmekuwa mkituma meseji zikinialika kutembelea duka la Vodashop lililo jirani nami ili nijipatie simu janja. Baada ya mwaka mzima wa meseji hizo kuwa kero, niliamua leo kutembelea duka na kuchukua simu yenu ili muendelee kufaidika na biashara yenu ya unyonyaji. Simu mnayouza kwa laki mbili faida yake ni laki moja, lakini siyo tatizo kwa kuwa ni malipo kidogo kidogo, buku buku kwa siku.
Nilipoingia Vodashop, muhudumu alinionesha bidhaa zenu na nilizipenda. Aliniambia nitoe namba yangu ili waone kama nakopesheka. Nilipomtajia, aliangalia kwenye mfumo na kugundua kwamba mimi siyo mtu wa mikopo, bali ninaweza kununua simu za bei kali kwa kuwa kwa siku nafanya miamala mikubwa. Kiasi cha kwamba ningeweza kukopa Samsung Galaxy 70 na kulipa yote kwa wakati mmoja. Muhudumu alizimia kwa mshtuko, nikamwagia maji ili azinduke. Alipozinduka, nikamwambia anipe masharti ya simu zenu.
Aliponiambia kuwa app za kubeti zimefungwa kwenye simu za mikopo na hazifanyi kazi hadi deni liishe, nilimwambia ameniambia jambo baya. Nikaamua sitaki kununua simu na nikaomba meseji zenu zisitumwe tena kwangu. Kwa sababu hela yenyewe ninayopata inatokana na shughuli za huko huko mlipofunga. Sikuona sababu ya kuendelea na mazoea hayo. Muhudumu alihuzunika kwa kunikosa kama mteja. Nilipotoka nje, nikakutana na meseji nyingine kutoka Vodacom ikiniomba nirudi dukani.
NB: Vodacom, simu zenu za mikopo zinatelekezwa na wateja hawalipi kwa sababu ya huu ujinga wa kufunga app za kubeti. Mmesikia uongo kwamba mkiruhusu app za kubeti kwenye simu zenu, watu hawatalipa mikopo yao? Msifanye makosa kama haya. Miamala mingi mnayopata inatokana na biashara ya kubeti. Mmefanya makosa makubwa na mnapaswa kutegemea hasara, kwa kuwa watu watazifungia ndani hizo simu.