Vodacom huduma za kifedha zimewashinda

nusuhela

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2014
Posts
5,915
Reaction score
7,210
Naomba niwe muwazi. Mimi ni mmoja kati ya watu wanaotumia huduma za kifenda za hii mitandao ya simu.

Naomba kuwapongeza tigo kwakua wako poa na hawajawahi kunisumbua.

Tatizo ni kwa hawa mpesa ambao ni vodacom. Kwakweli mnakela. Nimefanya malipo kwa selcom mgahawa mmoja pale mlimani city, hela imekatwa kwenye acc yangu lakini hakuna meseji iliyorudi kwangu wala risiti haijatoka kwenye ile mashine ya selcom pale mgahawani. Hili tatizo sio mara ya kwanza. Juzi nililipa jumia kwa selcom yao, pia meseji haikurudi. Meseji ilikuja kurudi kesho yake asubuhi.

Najiuliza, hivi ingekua nimelipa kwa watu nisio wafahamu ile juzi, ingekuaje??? Maana ukilipa kwa selcom, meseji ndo uthibitisho endapo risiti haijatoka kwenye kile kimashine.

Pia, leo nimejikuta nalipia mara ya pili kwakua nilikua nahitaji huduma.

Swali langu kwenu ni je, nitaipataje hiyo hela yangu???? Maana naamini kabisa kesho mtatuma confirmation message.

Kusema kweli, nimekua disappointed sana na nyie. Na ninasema kuwa huduma zenu bi za hovyo kabisa
 
Hawa voda ni ovyo kabisa mpaka mawakala wao wa m-pesa wanalalamika tu kibaya zaidi ukijiroga ukanunua umeme kupitia huu mtandoa token unaweza kutumiwa baada ya wiki ila tatizo limeanzia kwa huyu Director Mkenya
 
Hawa voda ni ovyo kabisa mpaka mawakala wao wa m-pesa wanalalamika tu kibaya zaidi ukijiroga ukanunua umeme kupitia huu mtandoa token unaweza kutumiwa baada ya wiki ila tatizo limeanzia kwa huyu Director Mkenya
Kweli tupu kuna siku nmenunua luku mpaka nimepiga mara 3 kwa customer care tofauti bila mafanikio mwsho ikaja moja
 
Vodacom wameyumba sana ndio maana nimestuka mapema na kuamua kuuza hisa zangu, kwa sababu huduma zimekuwa mbaya zitakimbiza wawekezaji na pia figisu ambazo zinaendelea kwa CEO mpya kwakweli ni kuwa makini la sivyo utakuja kukuta hisa zimefikia TZS 50
Huduma mbovu sana. Sasa kwenye data ndio balaa yaani hadi nikapeleka simu kwa fundi ila nilipobadilisha tu kwenye Halotel simu yangu kumbe ni nzima kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…