Vodacom imekuwa na desturi ambayo ni sawa na wale wa "ile hela tuma kwa namba hii"

Vodacom imekuwa na desturi ambayo ni sawa na wale wa "ile hela tuma kwa namba hii"

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
"NullYou have insufficient balance to subscribe the service. But you can dial *137*09*02 to subscribe the service via M-Pesa". Hawa nao ni wale wa " ile hela tuma kwa namba hii", nao wanastahili kukamatwa.

Vodacom imekuwa na desturi ambayo ni sawa na wale wa "ile hela tuma kwa namba hii", ujumbe huu nimeuona leo alfajiri 04:47 ukidai kama unavyosomeka, huu ni moja ya ujumbe ambazo zikidai nimejiunga na sijui nini eti kila siku nilipe shs. 2

00 vinginevyo nijitoe kwa kupiga sijui -----#! Huu ni mtego kwangu mimi kwani nikipiga kujitoa naona nitakuwa nathibitisha kuwa ni kweli nilijiunga ila sasa nimeshindwa mimi, siwezi kupiga kwani nawaona ni sawa na wale wa "ile hela tuma kwa namba hii".

TCRA, yapo malalamiko mengi yanayoihusu hasa kampuni ya mtandao wa simu wa Vodacom kuhusu kuchukua hela za wateja kwa hila, mfano, unaingiza namba za vocha ili ujiunge ghafla unapata ujumbe " salio halitoshi"! Kujiunga na kifurushi cha gharama ya vocha yako, wakiwa na maana wamekukata deni unalodaiwa wakati haujawahi kukopa, hata ukijaribu kuongeza salio jingine wanakata tena na kukutumia ujumbe wa "salio halitoshi"!

Mchezo huu ni wa miaka na miaka ukiambatana na malalamiko mengi kuhusu Vodacom lakini TCRA hamchukui hatua zozote kutulinda wateja dhidi ya utapeli huu. Baadhi yetu tumekuwa na hisia ya kudhani kuwa kampuni hii na nyinginezo zina mkono wa viongozi wa CCM ndiyo sababu hamuwakamati au hamuwachukulii hatu kutokana na malalamiko ya wateja. Uchaguzi unavyokaribia ndivyo kasi ya " umejiunga kifurushi cha kuwalipa shs. 200 kila siku" inavyoongezeka.

Ninamaliza kwa kuwataka TCRA mchukueni hatua dhidi ya uhalifu huu.
 
Namba ya 0738
Screenshot_20240502-074144.jpg
 
Natumia Voda, tigo. Sina tatizo la kukatwa salio.
Sbb nilizuia matumizi bila bando,, na kuna wakati wakawa wanakata sh 100 sijui ya nini. Nikawapigia voda wanitoe huko maana sijajiunga na chochote, til date sijawahi kukutana na hicho kitu
 
Voda wanachozingua ni kuwapata huduma kwa wateja kwa baadhi ya laini.

Mm nikiwapigia nasikia karibu vodacom dawati letu la VIP, for english press 1, au 0 kuendelea. Nampata muhudumu on the sport.

Ila kuna rafiki yangu akiwapigia, ni matangazo mwanzo mwisho hawapati. Mpk alinuna laini ya voda haweki salio zaidi ya kuichezeshea MKOBA
 
Airtel wanaweza kukuletea msg kuwa bando lako la yatosha limeisha au kifurushi cha internet kimeisha wakati unalo ukijichanganya unanunua kumbe bado unalo,yaani ni ujanja ili ununue wakati bado huhitaji.Kautapeli flani hv
Mi nshawazoea japo mara nyingi siungagi bando Airtel, sema hata tigo wana huo mchezo unakuta wakishakutumia ile 75% ya pili wanaanza kutuma sms zao za bando kwisha na wanakua wanatumia mara mbili mbili
 
Back
Top Bottom