Nawaandikieli
Member
- Aug 20, 2021
- 9
- 2
"Vodacom" Ngoma ikivuma sana, mwishowe hupasuka.
View attachment 1910929
Mbali na kuwepo mipango mingi ya baadhi ya watumiaji wa mtandao wa simu za mkononi wa Vodacom hapa nchini kuandaa wanasheria kwa lengo la kutaka kuifikisha kampuni hiyo mahakamani kwa kile wanachesema ni wizi kwenye vifurushi vya mtandao, limekuwepo pia suala la udanganyifu kwenye vifurushi vya jumbe za maandishi yaani MSG. Mteja ananunua kifurushi cha shilingi 3000 anaambiwa anapatiwa jumbe 10,000 ambazo atazitumia kwa kipindi cha mwezi mmoja, lakini jambo la kushangaza ndani ya wiki moja unatumiwa ujumbe kwamba "Umefikia ukomo" wa kifurushi husika.
Ni bora kama mmeamua kufanya udanganyifu, muwe makini. Mtumiaji akiangalia kama kweli ametuma jumbe 10,000, hapana hata 2,000 hazifiki. Katika hili mjitathimini kweli Vodacom kwani mnaweza kudaiwa pesa nyingi sana na wateja wenu pindi watakapoweza kupata CDR zao za namna walivyotumia vifurushi vyao. Mamlaka kama Mamlaka mnaweza msilijue hili pengine linafanywa na watumishi wasio waaminifu.