COURTESY
JF-Expert Member
- Jun 16, 2011
- 2,006
- 709
Nasikitika sana kuandika hii complain, maana imenifanya niichukie kazi ya uwakala wa vodacom m-pesa kutokana huduma mbovu nilizopata kutoka kwenye kampuni kubwa kama ya vodacom, kwanza customer care wana majibu mabaya sana kwa wateja hawajui adha tunazopata, sisi kama mawakala , una ripoti ishu yako mara moja ya kutuma fedha ki makosa wanakujibu usubiri ndani ya siku 7 hela inarudi, kwa unyenyekevu unakaa siku 7 hela yako iko hewani, then unawapigia simu mbona pesa haijarudi kirahisi wanakueleza subiri tena siku 7 hela yako inarudi! Are u serious unakaa na hela ya mtu 14days, tena wakala anaerisk maisha yake kukufanyia mnashindwa kumsaidia on time! Naomba kama kuna wahusika wa vodacom humu wajitahidi kubadilika kampuni imekuwa ya ajabu sana... Hela yangu kama itafanikiwa kurudi nachoma na laini.. Ntafanya kazi na tigopesa na airtel money tu