SMS ni njia ya mawasiliano. Tunazilipia hizo sms kwa kutambua kuwa ni kitu muhimu kwa mawasiliano. Lakini nadiriki kusema VODACOM wanatusumbua wateja kwa kutumia misululu ya SMS za matangaso kwa kuwa tu hatuwezi kuzikataa.
Nimeamshwa usingizini na ki-SMS cha kijinga eti narahisishiwa huduma za kibenki. Nimeamka simu ninaita kuna meseji kumbe Tangazo la biashara la Vodacom saa sita za usiku.
Hivi hakuna jambo sisi wateja tunaweza kufanya kupinga meseji za nuisense kama hizi mtu unaamushwa usiku ukidhani kuna jambo la muhimu kutoka kwa ndugu zako kumbe tangazo la biashara?
Ni kipi tunaweza kufanya kuondoa usumbufu wa aina hii?