VodaCom ni mali ya Serikali/CCM ama?

Chifunanga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
290
Reaction score
100
Hii mambo ya TRA kupokea malipo kwa kutumia M-PESA inamaana gani?

Ninavyofahamu mimi, M-PESA ni value-added service kwa Vodacom. Na kulazimisha au kushabikia wananchi walipie services za serikali kwa kutumia M-PESA ni kama kuifanyika matangazo/marketing Vodacom.

Kwa nini serikali isiseme watu watumie Mobile Banking Payments kwa ujumla na wana 'single-out' M-PESA peke yake. Vipi hizi nyingine? TIGO-PESA, ZAP, na ZPESA?

Voda imeanza kuwa kama mali ya CCM vile.....halafu sasa hivi ni nje nje yaani.....dah!.....TTCL imeishia wapi?
 
usiwaguse hawa walitusaidia sana kwenye uchaguzi please !
 
dah!! mkuu hapo umenena, halafu wanamtaka na mmiliki ajivue gamba, inawezekana kweli?
 
hata miee nashangaa kwanini wasingeweka hiyo huduma kwa TTCL,amabayo ndo ya kwao.kwanza inge saidia kuipa uhai,nyambaaaaaaaaafff....
 
hata miee nashangaa kwanini wasingeweka hiyo huduma kwa TTCL,
amabayo ndo ya kwao. kwanza ingesaidia kuipa uhai, nyambaaaaaaaaafff....

Watachekesha, kwa kuwa ni wao walioua sidhani kama wataweza kuwekeza tena. Wameua
kwa maslahi yao. Ni sawa na kumwambia Mramba afufue ATC wakati aliua ili kampuni yao isonge mbele
 
Magwanda kwa Kusengenya mko juu naona mmeanzisha bifu na Voda!
 
ROSTAM ametuzidi ujanja watanzania!kila sekta muhimu kakamata
 
Hili ni moja kati ya mengi.

Je hili la kuwalazimisha vijana wanofuatilia kupata mikopo ya elimu ya juu kwamba lazima wajiunge na Voda, then M-PESA then ndio waweze kulipia gharama za kuprocess, huu sio ubia mchafu ?

Ndio sababu naendelea kupiga kelele kila siku, kila saa, kila fursa, tunahitaji katiba ya watu, itakayotupa uwezo wa kutulinda na huu ufisadi

Wakati ni sasa!
 
aisee!!
sasa hawa watu wanalipa kodi kweli, nani wa kuwadai? any way tukiacha hayo share % zao ziko vipi? nani anaown nini? imekuaje wakapata deal nono namna hii?mbona imekuwa kimya kimya namna hii?
 
dah!! mkuu hapo umenena, halafu wanamtaka na mmiliki ajivue gamba, inawezekana kweli?

kwa huyo jamaa wanajaribu kujichuna ngozi, sijui kama maumivu yake wanaweza kuyamudu
 
Ila ni huduma nzuri inarahisisha sana. Wakati mwingine ukienda Bank kulipia unakutana na foleni kibao. Ila ndio utandawazi.
 
duh kweli bd tunawaza karne ya 20 wenzenu south africa kila kitu karibu waweza lipia via simu yako sasa mmeletewa ujuzi mnaanza kulalamika. unataka TTCL wapewe hiyo issue watu wangapi wanatumia ttcl? sio serikali iliyoleta hiyo issue ni VODA na marketing strategy zao wakapeleka propasal TRA km kawaida yao wakashangaa itawezekanaje wakapewa shule wakaelewa wakaingia contract. TTCL walikuwa wapi kuanzisha huduma km hiyo? hata hivyo hakuna monopoly kwenye hilo km wana technolojia ya kisasa wa implement hiyo huduma nao watapewa nafasi km vile luku ipo airtel voda nk.
 
Mali ya RA na EL!karamagi nae anaanzisha 4G mobile! SEACO mkonga wa taifa ni wa KARAMAGI na RA!
 
nilitaka kulalamika lakini nilipoona hizi picha za maiti hawa sina haki ya kuwaamulia waZanzibari kwenye maamuzi yao












 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…