nusuhela
JF-Expert Member
- Jan 26, 2014
- 5,915
- 7,210
Vodacom Tanzania kama mpo humu naomba hizi habari ziwafikie. Mimi ni mteja wenu mkubwa sana. Tena mteja kindaki ndaki. Sina line ya mtandao mwingine wa simu zaidi ya line hii moja iliyonayo. Ndugu zangu wengi wapo mitandao mingine, najitahidi kumudu gharama kuwasiliana nao ili tu nisiachana na nyie.
Sasa nasema basi. Huduma yenu ya #songesha imenifanya niwachukie sana. Haiwezekani niwalipe deni lenu lote alafu mshindwe kunipa mkopo mwingine. Hilo nimelikubali na nikaamua kuachana na huo mkopo. Leo nimetumiwa hela kwaajili ya mahitaji muhimu, mmekata tena hela yote wakati sina deni na nyie.
Hakika hapa nilipo nimekasirika hakuna mfano. Maana nimewasiliana na watoa huduma wenu, wananiambia changamoto itatatuliwa ndani ya masaa 96. Hii sio haki. Hata kama ni utaratibu mliojiwekea, lakini hii haikubaliki. Hela tunazotumiana kwenye mitandao hii ya simu ni hela za mahitaji ya haraka. Leo mnaweza sababisha mtu akafatiki kwa kuikosa hiyo hela yangu ambayo ilitakiwa ikafanye mahitaji ya muhimu.
Japa nilipo mpaka naogopa kuomba hela sehemu nyingine maana inaweza ikatumwa halafu ikakatwa nikaendelea kusubilishwa masaa 96.