Vodacom Premier League: Singida United yashindwa kufurukuta dhidi ya Simba SC, kwa kufungwa goli 1 - 0 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid

Vodacom Premier League: Singida United yashindwa kufurukuta dhidi ya Simba SC, kwa kufungwa goli 1 - 0 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania kuendelea kuvurumishwa leo Oktoba 27, 2019 ambapo Singida United wanawakabili Mabingwa wa Nchini Simba SC Mnyama Mkali Mwituni, kwenye dimba la Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

Simba SC, ambayo inaandika ushindi kwa asilimia 100% imejidhatiti kuhakikisha wanaendeleza na desturi hiyo ili kuweza kujikita zaidi kileleni. Je Singida United ataweza kuzuia moto wa Simba hii ya viwango vilivyothibitishwa na Shirikisho la soka Afrika CAF..Usikose ukaambiwa.

••Kulitaka Mwana..Kulipewa Mwana

tapatalk_1572180542086.jpeg
IMG_20191027_154339_166.jpeg
 
10' kuelekea dakika ya 12' 13 Simba wamelifikia lango la Singida Utd kwa shambulizi na kufanikiwa kupata kona ambayo haikuwa na matunda

Singida United 0-0 Simba SC
 
15' Vodacom Premier League uwanja wa Sheikh Amri Abeid, milango bado migumu..!

Singida United 0-0 Simba SC
 
20' Mashambulizi lango la Singida Utd huku mabeki wa Singida wakikaa vema.
 
Naam nakupata kwa uzuri kabisa mwalim kashasha naitakia simba ushindi wa goli mbili
 
Kona ya pili kuelekea lango la Singida United

Inapigwaaaaaaa, inapotea na kuokolewa..!
 
Mpira Leo mgumu Sana I naonekana mana simba kwenye VIWANJA vibovu hupat a matokeo hafifu
 
Kanda anakwenda sasa..Konaaaaaa, inapigwa na Ajibu inaokolewa vizuri na mabeki wa Singida Utd
 
Mchezaji wa Singida Utd yupo chini baada ya kupata rabsha..!

Singida United 0-0 Simba SC
 
Back
Top Bottom