Vodacom Premier League: Singida United yashindwa kufurukuta dhidi ya Simba SC, kwa kufungwa goli 1 - 0 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid

75' Simba kuna wachezaji wanapasha tayari kuchukua nafasi, Simba bado wako mbele ya bao moja
 
Aishi Manula na mchezaji wa Singida United, wapo chini baada kupata rabsha

Wameinuka mpira unaendelea
 
Aishi anasafiri na kuutoa mpira nje na kuwa kona..Inapigwa lakini na haikuzaa matunda

Singida United 0-1 Simba SC
 
Rashid anakosa nafasi ya kuipatia Simba bao la pili..Ilikuwa nafasi bomba..
 
Mpira umekwisha, Simba 1-0 Singida utd. Simba anaibuka na ushindi wa goli moja na point 3. Viva Simba SC. Goli la Simba limefungwa na Miraji Athumani
 
90+4' Kuelekea kumalizika kwa mtanange huu wa VPL

Naaaaaaaaaaaaaaam mpira umamalizika baada ya kukamilika kwa mchezo ambapo Simba SC imeweza kuibuka na ushindi wa bao moja bila majibu dhidi ya Singida Utd

Bao pekee limeweka kimiani na Miraji Athumani dakika ya 41 hivyo Simba imeendelea kujikita kileleni kwa alama 18 kwa michezo 6

FT: Singida United 0-1 Simba SC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…