Vodacom Premier League VPL' Lipuli FC dhidi ya Simba SC, Uwanja wa Samora Iringa

45+1' Kona kuelekea Lipuli FC, anakwenda kuchonga Chama Triple C, anapigaa

Naaaaaaam mpira ni mapumziko ambapo Simba wakitoka kwa kuongoza bao bila dhidi ya Lipuli FC

VPL, HT: Lipuli FC 0-1 Simba SC
 
HT: Simba imefanikiwa kumiliki mpira kwa kipindi cha kwanza, ambapo ilipelekea kupata bao
 
Kipindi cha pili kimeanza Uwanja wa Samora...VPL
 
Hatari lango la Lipuli, anakwenda sasa kwake Triple C, anamimina krosi kwa Boccoooo gooo laaaaaaaaaa

Ilikuwa nafasi tamu kwa Simba aaash
 
50' Shomari Kapombe yupo chini akipatiwa matibabu, ametoka nje, amerejea mpira unaendelea...!
 
55' Kameta lango la Simba, lakini Kennedy anakaa anaosha hatari ile

Lipuli FC 0-1 Simba SC
 
60' Kagere kwake Dilunga, anampasia Chama, aaah Simba wanatakata.

Namna gani Chama anakosa speed kuwahi mpira ule, ilikuwa movie kali sana Simba walifanya kuelekea lango la Lipuli.
 
Kenneth Masumbuko anatoka, na ameingia Issa upande wa Lipuli FC

Lipuli FC 0-1 Simba SC
 
Ile kasi imepungua na mpira unachezwa katikati ya Uwanja, huku kila timu ikitafuta namna ya kupenya kwenye lango

Lipuli FC 0-1 Simba SC
 
Kona inapigwaa kuelekea Lipuli FC, Inapigwaaaaaa na Chama, lakini Kichwa cha Kennedy kinashindwa kulenga lango.
 
Issa anakwenda hatari, oooooh Lipuli ilikuwa wapate bao baada ya shuti kutolenga lango
 
80' Ametoka Hassan Dilunga na nafasi yake amechukua Luis Miquissone upande wa Simba SC

Lipuli FC 0-1 Simba SC
 
87' Lipuli wanatafuta namna ya kusawazisha wanajaribu kulisakama lango la Simba, Lakini Simba wamejipanga vema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…