Vodacom Premier League 'VPL' Simba SC dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Uhuru

Mpaka ukirudi hautoshi kukaa kileleni tena Mtani.

Mzima lakini Mtani?
Ama kweli Chura FC hamtupendi, sare kwetu tu basi ndio mnashangilia mpaka sauti zinawakauka!

Hebu kwanza nipe msimamo wa ligi nani yupo mkiani na nani yupo kileleni? Halafu ndio tutaongea baada ya hapo,
 
Hivi nyinyi na sisi mwaka huu.
Nani alikuwa anachonga sana.

Hahahaaa mmesahau mlikuwa mnapokeana kwa mbwebwe airport


Ngoja tusubiri ya korosho city uko Leo
Usimcheke mamba kabla hujavuka mto
Hahahaa. Leo bao moja tu linawatosha hao walima korosho Mtani.

Kama nawaona Mtani mtakavyokuwa mnakodoa macho huku mkiombea tupoteze. 😀😀😀
 
Ama kweli Chura FC hamtupendi, sare kwetu tu basi ndio mnashangilia mpaka sauti zinawakauka!
Tunaachaje kukaukwa na koo sasa. 💃💃
Hebu kwanza nipe msimamo wa ligi nani yupo mkiani na nani yupo kileleni? Halafu ndio tutaongea baada ya hapo,
Msimamo utakufaa sana pale tutakapokuwa tumecheza mechi sawa Ses.
 
Sawa mbumbumbu ashakusikia
 
Aiseee mbona mapema hivi Mkuu?
 
Aiseee mbona mapema hivi Mkuu?
Kaniudhi Sana Jana, kila faulo za karibu na Goli anakimbilia kupiga halafu anapaisha zote.
Najuiliza hivi kwanini anapoteza kwa makusudi nafasi za magoli ?
Kwanini anakimbilia kufanya kitu ambacho hakifanyii mazoezi ?
Kwa umri wake na muda wake wa kucheza mpira hakustahili kucheza kwa kiwango hicho.
Hivi hakuna wapiga faulo kabisa ?
Kaniudhi Sana Jana.
 
ingawa chura wamevamia uzi wetu haitunyimi nafasi sisi Simba kujadili timu yetu, Ajibu ni mchezaji wa media sielewi ni kitu gani Simba walimchukuliakwa sababu Simba haina tatizo na wachezeshaji mara nyingi anapooza move wakati timu inashambulia anapooza mpira kwani lazima atulize na kuanza kufanya madoido kwa timu yenye nidhamu ya ulinzi kama Prison huwezi kuwafunga maana wanarudi haraka na kuziba nafasi, Shabalala bado anarudia makosa yake ya kupenda kushambulia na kuchelewa kurudi kukaba magoli mengi tuliyokoswa koswa yalitoke upande wake na pia anapopata mpira wakati mwingine analazimisha kupiga chenga wakati anajua uwezo wake wa kupiga chenga ni mdogo kocha awe makini anapofanya mabadiriko Dilunga hakutoa mchango wowote alipoingia kipindi cha pili pia sio lazima Kagere amalize siku zote na atengeneze mfumo wa kuwa na washambuliaji wawili kumtegemea mshambuliaji mmoja Kagere peke yake ndio kulituponza tulipotolewa na ile timu ya Msumbji
 
Issue kubwa ni kuwa wachezaji Simba wapo ila kocha hakuna.

Angekuwa kocha mwenye uwezo mzuri angeweza kutengeneza timu mbili very strong, ila kwa sasa bado anastruggle na hiyo timu moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…