Vodacom Tanzania: Kwanini mnataka kunisitishia huduma ya kukopa M-PAWA halafu tena mnaniuliza kama ninahitaji mkopo?

Nilikopa tuela twa mboga basi ikawa nongwa. Niliandikiwa ujumbe wa kunitishia kupelekwa polisi kwa kosa la wizi wa kimtandao. Pamoja na kuomba muda ili nimalizie deni, barua za vitisho ziliendelea kuletwa kwangu. Nilimaliza deni hilo na sasa kila baada ya siku moja naletewa ujumbe ukiniomba nichukue mkopo toka M-Pawa. Niliapa kwa MIFUPA ya babu zangu, "kamwe sitakopa tena tuela twa mboga toka kwa hawa jamaa "mashailoki".
 
Hee barua tena,,inakuja vip hiyo barua?
 
Majizi hao, siku hizi ukikopa elf 20 wanakata 3,500 hapo hapo na unarudisha ndani ya mwezi. TCRA wapo tu wanaangalia, wale wanaoweza ku-calculate riba tunaomba mfanye mahesabu hapa.
 
Hii message iliingia kwenye simu yangu nikiwa ninakunywa chai. Hauwezi kuamini nilicheka mpaka nikataka kuangusha kikombe cha chai chini...
Mkuu, mimi walinipa vitisho vingi sana, ila badae wakaniletea mpawa, kuna siku niwezeshe tena, nikakosa aaahhhh Hadi najiuliza hivi Hawa watu wakoje?

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Dawa ya deni ni kulipa...
Nimewalipa pesa yao yote jana.

Sasa vp kuhusu integrity pamoja na umakini wao katika kazi? Kama computer systems zinashindwa kutofautisha mteja aliye mdaiwa na yule asiye, kwanini tusiamini kwamba ipo siku watatuongezea madeni yetu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…