Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

VODACOM.
Namba zangu za simu ni 0755519736
siku ya leo simu yangu ilikuwa na salio la 250 na nikakatwa 83 sh/ Na hivyo ikabaki sh 167 nimeongea na vodacom huduma kwa wateja na kuwaeleza tatizo langu la salio kukatwa na hadi muda huu sijapata muafaka wowote,wakti salio langu limekatwa simu yangu ilikuwa na MB,DAKIKA na SMS.
Majira ya saa 11:19:37 pm nikapata sms ilokuja na jina REMEDY,Napenda kuicopy sms hiyo hapa :
"Ombi lako limepewa namba CSR118369841. Tutakujulisha punde tu litakapotatuliwa. Asante kwa kuchagua Vodacom."
mpaka muda huu salio langu halijarudi na nimeongea tena na kituo cha huduma kwa wateja na jibu nilopewa si la kuridhisha.
Napenda kuwauliza voda ni lini na saa ngapi mtarudi pesa yangu mlokata au ni mfumo mpya wa kutuibia wateja wenu ?
Nategemea jibu mtanipa kupitia namba yangu ya simu kwani sitoweza kuingia tena ktk mtandao wa internet kwa kuwa salio langu lishachukuliwa.
NYONGEZA:mimi nipo mkoa wa Arusha.
 
Hata mimi niliweka airtel unlimited ya mwezi mara baada ya siku kama tano nashangaa wananitumia mesej hii " Your service may be degraded as your usage is abnormal. Internet sharing/tethering from your device is not allowed.
Huduma yako ya interneti itaathirika kwa sababu matumizi yako sio ya kawaida .Kutumia kifaa hiki kuuganisha vifaa vingi hairuhusiwi."
Nkajiuliza hawa jama a wana akili kweli mana huo utaratibu/ sheria mbona hawakuniambia. Wanakaa na sheria zao mfukoni alaf zinaingia kwenye utendaji kihini. Hii pia ni wizi wa wazi. Mpaka sasa hiv internet yangu imekuwa slow mpaka basi. Na nmeshasitisha kutither. Nnampango nihamie mtandao mwingine
 
Tatizo la Voda nikwamba kunabaadhi ya number zatigo ukizipigia ukiwa umejiunga na Bando la mitandao yote haziendi kama bando zinatumia pesa iliyondani ya simu , kama imeshindikana kabisa turuhusuni wanachuo tulitafutie ufumbuzi tatizo hilo
 
nyie jamaa hebu rekebiseni hiki hili suala la kutuwekea SMS nyingiiiii kwenye vifurushi baadala ya MB jamani,dunia hii tunatumia zaidi MB na sio SMS badirikeni
 
Voda wababaishaji tu natumia Zantel sina stress kabisa mb125 DKK 20 mitandao yote kwa 500 tu
 
Vodacom! ukweli nawakubali kwa huduma znu,lakni mimi nipo kwenye huduma ya cm swop ukweli mumeifanyakuwa ngumu sana mpaka sasa hvi watu wanaogopa kuswap laini za voda.Hebupunguzeni idadi ya maswali mimi mwenyewe ninayo huduma hyo kwakutumia hii laini yangu,lakni had sasa nina 3 months cja swap zotezinagoma kwa sababu ya maswali yanakuwa magumu wateja kuyajibu.Nibora huduma ya kupiga cm,nina mengi ya kusema lakni nasubiri ufuatiliaji wenu.
 
Kila siku nawaambie network inazingua sana hakuna cha 2 wala 3g hata h wala e sasa what are you doing nyie au mnataka tuhamie tigo?
 

Ahsante kwa mrejesho Mlima Meru, tunaaamani unaongelea huduma ya My Number1 ambayo kwa sasa inafanyiwa marekebisho, itakaporejea tutafahamishana. Ahsante
 
Sorry Guys its with regret that what appearing waw no my intention and working on how to delete it
 
Habari mkuu, yale si matangazo ni maelekezo/maelezo ya awali ya jinsi ya kutatua tatizo linaloweza kuwa linamtatiza mteja. Ukihitaji msaada wa haraka unaweza kupiga namba 15366.
 

Ahsante Jitaboy, tungependa kufahamu maswali gani yamekuwa magumu zaidi kwa wateja. Karibu
 
Kwa hilo mi naunga mkono ondoe ni uduwanzi ule ukiona nimepiga ujue na tatizo sasa kuanza kunipitisha mbagala nikunje kona mpaka ilala wakati mi naenda posta straight sio nzuri mtu akipiga pokea na si kuanza kumzungusha zungusha
 
Pole sana, tafadhali tutumie namba ya simu PM kwa msaada zaidi.
 
Tatizo la Voda nikwamba kunabaadhi ya number zatigo ukizipigia ukiwa umejiunga na Bando la mitandao yote haziendi kama bando zinatumia pesa iliyondani ya simu , kama imeshindikana kabisa turuhusuni wanachuo tulitafutie ufumbuzi tatizo hilo
Habari mkuu, tafadhali wasiliana na kitengo cha huduma kwa wateja namba 100 endapo utapata tatizo hili tena kwa msaada wa haraka. Pole
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…