Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Nimenunu Simu Itel 2060 Kwenye Duka La Wakala Wenu Delta Africa
Sasa Hii Simu Wakala Kaniambia Niende Sehemu Ya Ujumbe Niandike Neno ZAWADI
Halafu Nitume Kwenda Number 15300
Ili Nipatiwe Zawadi Ya Dakika 550,Mb 500,Sms 3000

Nilifaya Hiyo Kwa Kutumia Simu Niliyonunua
Yenye IMEI:356393074132225
Baada Ya Muda Nikajibiwa Kuwa IMEI Haitambuliki.

Nikaona Nipige Simu Dawati La Msaada La Vodacom Aliyenipokea Nikamueleza Tatizo Langu Kuhusu Zawadi Zilizopo Kwenye Simu Niliyonunua Na Zawadi Zilipomo Na Ambapo
Nilipotuma Ujumbe Nimejibiwa Imei Haijulikani.

Sasa Nilitaka Anieleweshe Hii Simu Ina Hizo Huduma Ama Haina Cha Kushangaza
Anasema Nirudi Dukani Ambapo Simu Nilinunua Shoppers Msasani
Nami Naishi Kivule

Nikamuuliza Nitarudije Dukani Wakati Hii Zawadi Inatolewa Na Vodacom Kwa Kufuata Maelekezo Anasema Rudi Dukani


Nikamuuliza Nieleweshe Je Hizo Zawadi Zinatolewa Ama Vp Mtoa Huduma Kwa Mteja Anasema Hajui

Hivi Simu Mfano Umenunua Dar Unakwenda Kigoma Urudi Dar Kufuata Zawadi Ya Dakika Ujumbe Na Mb

Vodacom Kuweni Wastaarabu Hasa Customer Care Mna Majibu Yaliyojaa Ukakasi Sana
Ni Mimi 0756457061
 
Hili tangazo la SIMUtv limenichosha. Kwa siku mara tano. Naomba ushauri jinsi ya kuondokana nalo kwa vile limekaa kama kirusi fulani vile.
 
MTANDANDA WA VODA KWA SASA NI WA USUMBUFU MNO. NIMETUMA PESA SHILINGI 100,000/- KWENDA KWENYE KAMPUNI FULANI. LEO SIKU YA NNE PESA HAIJAFIKA NIKIWAULIZA VODA WANASEMA PESA YANGU IKO HEWANI. WANAJAMVI EBU NIELEWESHENI PESA KUWA HEWANI MAANA YAKE NI NINI?
 


UMEPIGWAAAA HAKUNA CHA PESA KUWA HEWANI
 
Naomba kuondolewa kifurushi cha buku ten kwa siku saba nirudishiwe
Kile cha buku siku tano mm sio menager wa bank maana mmekiweka coz nilikuwa najiunga sana mkajua nafanya kazi bank
 
Habari wana jukwaa?
Vodacom Tanzania wana application ya simu ya M-Pesa. BIG UP sana kwa hili maana katika dunia ya sasa ya digitali tunahitaji huduma muhimu kama hii iwe katika kiganja.
Ukakakasi unakuja kwenye jambo moja; app hii haifanyi kazi vizuri. Nimeinstall kwenye simu yangu ila haifanyi kazi kwa Wi-Fi inataka utumie mobile data. Ila hata ukitumia mobile data haifanyi kazi. Nimepitia review nyingi za watumiaji wa app hii wanalalamikia tatizo hilo. Sasa Vodacom Tanzania jaribuni kutatua hili tatizo kwa kurekebisha app yenu maana haina siri nyie ndio mnaongoza kwa wateja katika huduma hii ya kifedha.
Wassalam!
 
Pia mobile data wanataka iwe ya voda tu yaan kama una access kwa data za mtandao mwingne haitaki
 
Inaboa. Wameharakisha sana kuiweka sokoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…