Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

vodacom m pesa mnahuduma mbovu sana. leo nilikuwa najaribu kutoa pesa kwa wakala chakusikitisha wakala ananiambia hakupokea msg kutoka makao makuu.

ikabidi nikae zaidi ya masaa 6 ndo wakamtumia msg wakala ili atoe pesa. huduma zenu mbovu sana hapa wilaya ya hanang eneo la cmsc
 
Minara yenu IPO tu huku visiwa vya ziwa Victoria lakini mawasiliano ni shida mno, internet ndiyo taabu kabisa Sikh zote network busy.

Nazungumzia mnara wa MAISOME ISLAND, Mbona mnazidiwa na Airtel ambao kwayo nyote minara yenu na yao IPO eneo hilo hilo, hata hapa natumia airtel, Voda yenu imebuma!!!
 
Mimi Niko wilayani Rombo hususan mnara wa Hakwe. Siku za nyuma internet ilikuwa nzuri sana lakini baada ya voda kuongeza mnara wa Ngoyoni imekuwa ya shida na ya kuoteaotea. Shida ni nini?
 
Samahani nilipumzika kwa mda kutumia Till yangu ya mpesa baada ya kuibiwa. Haikufanya muamala wowote kwa Muda WA mwezi moja lkn ilikuwepo hewani na ina salio ndani.

Sasa nilihitaji kuitumia tena nakuta haina menu ya m-pesa nikaenda Voda shop naambiwa imefungwa mpaka niende Dar es salaam makao makuu na mm nipo mkoani. Mtanisaidiaje kutatua tatizo langu?
 
Hivi Voda mna matatizo gani kuchukua pesa mko fasta ktk akaunti yangu lakini Huduma sifuri, Jana nimenunua umeme wa luku kupitia M-PESA lkn hadi sasa naandika SMS hii sipata token na pesa mmechukua huu ni WIZI iweje sms za matangazo yenu ziwe zinafika fasta mara app sijui jiunge na miito

ila kila nikipiga Huduma kwa Wateja mnasema pesa yangu iko hewani mbona hayo mabango yenu hayakai hewani yanafika fasta, mna bore si mara ya kwanza, rudisheni pesa yangu huko mnaiona,..
 
swali langu ni kuhusu M pawa je? ni vigezo vipi munaangalia ili kumpandisha mteja kiasi cha kukopa?
 
Hivi Hua mnajibu Maswali kweli???


Haya mimi swali langu ni hivi ubao wa DSE Tanzania hampo mpaka sasa na tarehe 12 June 2017 ndio ilikua ck ya nyie kuwepo at first time baada ya kuuza share zenu, tupeni feedback kwanini hampo hadi leo???
 
Hivi Hua mnajibu Maswali kweli???


Haya mimi swali langu ni hivi ubao wa DSE Tanzania hampo mpaka sasa na tarehe 12 June 2017 ndio ilikua ck ya nyie kuwepo at first time baada ya kuuza share zenu, tupeni feedback kwanini hampo hadi leo???
Ukitaka wakujibu hawa. Leta mada kuwa wanahusika na makinikia labda.
 
Suala LA HISA linaendeleaje? Has a wale walionunua kupitia Benki...tupeni mrejesho..
 
hivi nyie voda mbona hamtaki kuwajaza wateja wenu kama tigo wanavofanya
 
wanasumbua ila Sio kama tigo
 
shitaki kama una evidence
 
Kwa nini mnatuuzia tablet kwa bei kubwa halafu hamna spea zake?

Mfano,mtu bahati mbaya amevunja kioo cha tablet,kwa nini vioo vyake hamuuzi/kwanini vioo vyake havipatikani? Je mnatuuzia kwa makusudi?
 
Ndg Mteja una deni la 805 Tshs kutokana na huduma za Nipige Tafu. Tafadhali ongeza salio ili kulipia huduma hii. Vodacom Kazi ni Kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…