Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Pumbavu kabisa laini zenu za m.pesa mmegeuza deal la wafanyakazi wenu ngoja ttcl ikue muone
 
VodaCom mmejisahau sana! Mtandao hata wa kutuma sms kwa baadhi ya maeneo ni hamna kabisa! Maeneo ya manyara barabara kutoka katesh kwenda kondoa(dodoma) ni hakuna kabisa mtandao lifanyieni kazi basi
 
Jinsi gani naweza pata ubia wa kuuza mashairi yangu ya kiswahili na kiingereza kupitia vodacom?
 
Mimi ni Mwanahisa wa Voda ni muda mrefu sijapata gawio tangu niwekeze, kulikoni?.
 
Mbona hamjibu watu tunaibiwa helaa mna msaada gani sasa transaction inafanyika bila mtu kujua???
 
mnaonaje mkianzisha hudama za pesa mfano kununua dollar,euro n.k kupitia m pesa..?
 
Voda mpesa kunatatzo gni dar mbn miyeyusho watu namatatz ytu tunatatuajee [emoji37][emoji37][emoji37]
 
Habarini wadau!
Nimeamua kuandika hii thread kupendwa kujuzwa na wadau kama vodacom ni wezi au la?

Nimekuwa natumiwa message kila siku ya tusua mapene ya kushinda milioni 100 kila siku na nimekuwa nikicheza mara kwa mara lakini sijawahi sikia mtu anashinda hiyo milioni 100 kila siku kama wanavyojitangaza.

Na kama hamna mshindi wa milioni 100 kila siku, huu si uongo wa kuvutia watu wacheza bahati nasibu huku wao wanakula tu hela. Au ndo kurecovery techniques baada ya kupata loss ya bilioni 350?

Naomba kuwasilisha.
 
Inatia hofu maana hatujawahi kusikia hata mmoja aliyeshinda hiyo M100, pia hata hao wanaoshinda hizo ndogo wanaandika majina yao kwa mkato tu kwani wanaogopa nini kuyatangaza mbona tangazo la kushiriki wanalitoa kwanini wakwepe kutangaza washindi?
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu.
Jana saa kumi na mbili na dakika sita (12.06) nilijiunga kifurushi cha Yakwako Internet cha masaa 24, leo saa nane na dakika thelathini na tatu (8.33) wananitumia sms kwamba kifushi changu kimekwisha muda wake ( sio kimeisha kimatumizi), sasa huu si wizi na utapeli juu ya pesa yangu niliyonunulia kifurushi cha saa 24.

Na nimejaribu kuwasiliana na huduma kwa wateja, nako ushirikiano wao ni zero kabisa.

Yan aisee MB zangu zimenuima kweli!

Voda nyinyi hivi ni lini mtaacha huu wizi na utapeli + uhuni kibao??.
 
Hbari za leo niliishajitoa kwenye huduma ya kupokea matangazo kutoka vodacom kwa ujumbe wa maandishi. Nasikitika kupokea matangazo ya kamari inayoitwa mojabet.
 
Kwa mtazamo wangu nadhani voda mmezidiwa wateja.kwenye enternet kwenye miamala ya kifedha mko vizuri ila
 
Hili swali linahitaji majibu ya kina, tena kwa haraka...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…