Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Yaani Vodacom mnaboaa jamani internet iko slow na inakatakata kila mda najuta kununua line yenu niko mbioni kuitupa
 
Bei zenu za vifurushi bado vipo juu sana hatari. Bora mpunguze Meseji lakini MB ni ziwe nyingi za kutosha
 
Vodacom Tanzania, chonde chonde hatuhitaji kufanywa bango la matangazo au simu zetu kugeuzwa chombo cha kuhifadhi meseji zenu zisizo na kikomo.

Please tuondoleeni hii kero ya kututumia ujumbe kila baada ya dakika kadhaa kuhusu matangazo yenu, tena mnatuma hata mara tatu au nne kwa siku ujumbe uleule mmoja, halafu utashangaa ujumbe huohuo unatumwa kila siku. Kiukweli siku hizi mmenifanya kila nikiona ujumbe wenu huwa hata sisomi kujua kuna nini bali naufuta mara tu ukiingia, ukweli mnaboa sana.

Mimi ni mteja wenu tangu mwaka 2002 na namba ninayoitumia sasa ninayo tangu mwaka 2004, lakini imefikia hatua nataka kuhama maana mnaboa.
 
Mimi ushauli wangu kuhusu sms tunazotumiwa na voda ambazo atujaziomba wazipunguze zinatumalizia chaji za simu zetu
 
Mimi.nimeshulumiwa 150000 na mfanyakazi wa Vodacom Geita na hataki kunilipa pesa zangu.naombeni mawasiliano ya Vodacom.Geita nisaidiwe kupata pesa yangu.
 
INSTAGRAM BURE! Angalia/Post Picha Insta bure, pamoja na GB 2 za intaneti utumie kwa saa 24 kwa Tsh 3000 tu!. Piga *149*03#.Vigezo na Masharti kuzingatiwa



Eti mpo serious na biashara au ni samasoti baada ya shibe??
 
Vodacom Tanzania Mnazingua Sana kupata Statement ya Mpesa ni elfu saba kwa kila mwezi ina maana kama unataka ya miezi 12 ni elfu 84. Na wakati wenzenu tigo Buku Jero tuu unapata ya mwaka mzima

Tuhurumieni basii sisi wateja wenu mmetunyonyaa sanaa aisee
 
Hata Mimi tatizo hili limenikuta sana yaani mpka najitumia SMS mwenyew na line nyngne lkn waap haiji
 
Vodacom ndo mtandao wangu pendwa, actually mko vzr mengine ni mapungufu madogomadogo ambapo kila sehem(mtandao wa simu) yapo ILA sasa napenda tu nishauri kuwa kuwepo na shortcut kwenye menyu ya kuzuia muamala hata Kwa Mimi muhuika pasipo kuanza kuklpiga simu hudum Kwa wateja na pengine isipokelewe Kwa wakati, ingawa pesa haipotei kirahisi lakin tu katika kuweka wepesi wa huduma fanyeni kiturahisishia mlolongo wa hudumu ya kipesa (mpesa) hata tukikosea kufanya muamala.

Ahsanteni sana Kwa huduma yenu ilotukuka!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi inawezekana kulipa mkopo wa M-pawa then muda huohuo ukaomba mkopo kiasi kikubwa zaidi ya mwanzo.??

Sent using Jamii Forums mobile app
Salaam Nanga,
kuongezeka kiasi cha kukopa inategemea na mwenendo wako wa matumizi ya simu na kufanya marejesho, na si rahisi ikawa ghafla. Endelea kuwa nasi kwa huduma nzuri zaidi.
 
shukrani sana Kibomonya,
Tutazingatia ushauri wako. Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…